Kazi Nzuri Sana – Kama Unaweza Kuipata!

Februari 25, 2015

Kuendelea na mlolongo wa matamko, Msimamizi wa Benki Kuu, Dinos Christofides, ametoa tamko kwa mameneja na wafanyakazi wa FBME tawi la Cyprus kuwakumbusha kwamba muda wa kawaida wa kufanya kazi tawini kwa siku ni 2:30-11:00. Pia aliongeza kuwa mfanyakazi mwandamizi yoyote anyetaka kwenda likizo anatakiwa kupeleka maombi yake kwenye idara ya Wafanyakazi na kubiri kupata kibali cha Mr Christofides .

“Hii itatumika kwa kila mmoja kwenye tawi la Cyprus “bila upendeleo”, anaandika. Kwa kweli, anasema ‘bila upendeleo’ lakini ni wazi kwamba haimhusu Mr Christofides mwenyewe, ambaye anaondoka kila siku saa 8 na kupotelea kusikojulikana, na kusababisha miamala ya tawi kusimama na kuchukua likizo za dharura na kwenda sehemu zisizojulikana. Kwa hili, anajilipa mshahara mnono kutoka fedha za Benki ya FBME. Kazi nzuri sana hii kama unaweza kuipata!