Bunge la Cyprus Laahirisha Usikilizaji

Februari 20, 2015

Mjadala kwenye Baraza la Wawakilishi – Bunge la Cyprus –kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus dhidi ya FBME, ambao ulikuwa umepangwa kusikilizwa Jumanne iliyopita, tarehe 17 Februari, umeahirishwa kwa ombi la Mwanasheria Mkuu wa Cyprus, Costas Clerides. Katika kukubaliana na ombi hilo, wajumbe wa kamati ya Bunge waliopangwa kusikiliza shauri hilo wameweka wazi kwamba litasikilizwa siku za usoni.

Kulingana na barua ya Februari 11 kutoka kwa Mwanasheria Mkuu iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari, Mr Clerides aliomba kuahirishwa ili kuzuia kuibuka kwa mambo yanayoweza kusababisha matatizo kwa Serikali katika kesi ya madai kwenye mahakama ya Cyprus na pia kwenye mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi, ICC mjini Paris. Pia alikataa kuhudhuria kikao yeye mwenyewe. Ni wazi kwamba yupo kwenye nafasi ngumu ya kuangalia maslahi ya asasi za serikali pamoja na yale ya kisheria na matendo ya viongozi waandamizi.

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Aristos Damianou MB, amekuwa akinukuliwa kwenye vyombo vya habari nchini Cyprus akisema kuwa wakati kamati haipendi kuumiza maslahi ya Serikali, lakini maamuzi yake hayawezi kuchukuliwa kama ahirisho la muda usiojulikana.

“Kinyume chake,” alisema, “wale waliohusika wakati wa kushughulikia suala hili wataitwa kama sehemu ya udhibiti ya bunge, kuwajibika kwa matendo yao, kutokuchukua hatua au makosa mengine.”

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya Bunge, Mr Damianou aliongeza kuwa wabunge hawataki “… mjadala wowote wa bunge kujenga Dhamira potofu kwa matendo yaliyotokea siku za nyuma kwa taasisi yoyote … hata hivyo tuna mashaka na jinsi uongozi wa taasisi ya Umma ilivyolishughulikia suala hili (la FBME) ambalo linaweza kuigharimu Serikali mamilioni ya fedha “.