Mahakama ya Wilaya ya Marekani Yaweka Zuio la Mwanzo dhidi ya FinCEN na Maamuzi yake ya Mwisho.

Agosti 28, 2015

Mnamo Agosti 27, Mahakama ya  Wilaya ya Columbia, wamekubali kuweka pingamizi la awali dhidi ya FinCEN na washitakiwa wengine wa Marekani na kuzuia Maamuzi ya Mwisho ya FinCEN yasifanye kazi hadi hapo Mahakama itakapotoa humumu yake ya mwisho, kama ilivyoombwa na FBME Limited na  Benki ya FBME Limited. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye amri ya mahakama kwakubofya hapa.

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Jacob Ley, Katibu wa idara ya  hazina ya Marekani,  Jennifer Shasky Calvery_ Mkurugenzi wa FInCEN and FinCEN yenyewe.

FBME itatoa taarifa kila mara tunapopata taarifa mpya kuhusu maendeleo ya kesi hii.