Uamuzi wa FinCEN Una Makosa Mengi ya Ukweli na Kisheria

Julai 27 2015

 FBME Limited imeisoma hukumu ya mwisho ya Taasisi ya Kuangalia Makosa ya Kifedha ya Idara ya Hazina ya Mrekani (FinCEN)  iliyotolewa tarehe 23 Julai 2015, na kutoa taarifa ifuatayo:

Uamuzi wa FinCEN hauwezi kuachwa kukosolewa. Ingawaje Benki na washauri wake walifanya juhudi kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuelezea mifumo ya kupambana na fedha chafu AML na uendeshaji,  miamala na shughuli nyingine, makosa makubwa ya kisheria na upotoshaji wa ukweli yaliyomo kwenye hukumu hiyo ya mwisho inaonyesha kwamba iliandikwa na watu bila kutilia maanani maelezo muhimu tuliyowapelekea sambamba na nyaraka nyingine walizokwisha kuwa nazo.

Benki inakusudia kutafuta njia yoyote inayowezekana kujilinda ipasavyo dhidi ya udhalimi huu kwa kufungua kesi kwenye mahakama ya Washington DC dhidi ya Idara ya Hazina ya Marekani.

Taarifa zaidi zitatolewa katika wakati muafaka kupitia tuvuti hii ya www.fbmeltd.com