Desemba 11, 2015
Benki ya FBME imepinga vikali ushahidi uliotolewa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) unaodai kwamba iligundua mapungufu katika mfumo wake wa kupambana na fedha chafu AML na CTF na inaangalia uwezekano wa adhabu ya kisheria inayotolewa na CBC.
Aidha, FBME inaona kwamba hii ni hukumu iliyotengenezwa kulingana na ukaguzi wa CBC-uliofanywa wakati wa majira ya joto mwaka 2014. FBME inauliza kwa nini imewachukua CBC karibu mwaka mmoja na nusu kutangaza matokeo haya ya ukaguzi? Hali hii inatuelekeza kwenye ukweli kwamba Idara ya FinCEN nchini Marekani imebidi iongeze kipindi chake cha kukusanyika na kutathmini ushahidi hadi mwisho wa Januari 2016 baada ya mahakama ya Marekani kusitisha jaribio lake la kutoa hukumu ya mwisho dhidi ya Benki ya FBME, inasemekana kamba kitendo hiki cha utoaji holela wa matokeo ya ukaguzi na CBC na FinCEN yana uhusiano wa moja kwa moja.
FBME inabainisha kwamba mapungufu waliyoyataja yanahusiana sana sana na taratibu na sio miamala ya fedha ndani ya Benki ya FBME. FBME pia inathibitisha kwamba kauli ya CBC inapingana na matokeo ya uchunguzi huru uliofanywa na kampuni ya ukaguzi ya Kimataifa ya Ernst and Young (E & Y) inayoongoza nchini Marekani, na ukaguzi uliofanywa mwaka mmoja uliopita na kampuni ya KPMG ya Ujerumani. Baadhi ya yaboresho ya mifumo yalipendekezwa ili kujiweka vizuri katika viwango vya kimataifa na hakuna kampuni iliyoona ukiukwaji wowote wa sheria na maagizo ya EU na Cyprus.
Kaguzi hizi, ambazo matokeo yake yamepelekwa FinCEN, yanathibitisha kwamba FBME inakidhi taratibu za kisheria na mahitaji ya Umoja wa Ulaya kuhusiana na kupambana na fedha chafu, agizo la tatu la AML na toleo la nne la mwongozo wa Cyprus ‘kwa mujibu wa Ibara 59 (4) ya Jamhuri ya sharia ya kupambana na fedha chafu’. Aidha, Ernst and Young pia walitoa taarifa kwamba FBME “… ina mfumo maridadi ambao unairuhusu Benki kuendelea kukidhi mahitaji ya kisheria.