Wenye Hatia Ni Nani?

Desemba 24, 2015

 Tangia Julai 2014, mwanzo wa sakata lake dhidi ya Benki ya FBME, Benki Kuu ya Cyprus (CBC) imewapeleka wadau kwenye mlolongo wa kushangaza wa vitendo visivyo na mantiki vilivyoibua maswali muhimu kuhusu uaminifu wake kama chombo cha serikali katika siasa za kisasa za Ulaya. Kwa kipindi kirefu cha miezi hii 17, CBC ilikuwa kimya kueleza nia yake, na ni hivi karibuni tu ndio wameanza kuonyesha ukweli wa yale yaliokuwa yakiendelea nyuma ya pazia, na hii ni dalili ya kushindwa kwenye vita vya kisheria kwenye midani ya kimataifa.

Hatua ya hivi karibuni ya CBC ilikuwa ni kufuta leseni ya FBME tawi la Cyprus. Tangazo fupi kwenye tovuti ya CBC halikutoa sababu, lakini viongozi wa FBME walitambua baadae kwamba sababu iliyotumika ni kwamba tawi haliendesheki. Kitu ambacho CBC hawakisemi ni kwamba kutoendesheka huku ni kutokana na kitendo cha CBC kulipoka tawi mnamo Julai 2014, na kuliweka katika hali tete tangu wakati huo.

Kuanzia siku ya kwanza, maamuzi ya CBC ya yalikwenda kinyume cha sheria za Ulaya (EU) na Cyprus na kuonekana kabisa kulikuwa na ajenda ya siri.

Imetoa madai kwamba FBME imeruhusu kutumiwa kusafisha fedha chafu, ingawa ushahidi kutoka wakaguzi huru unakinzana na hoja hii. Wakati haina nukuu yoyote inayounga mkono shutuma zake, ni vema kutamka wazi kuwa taarifa za uchunguzi uliofanywa kwa FBME na wataalamu wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na wale walioteuliwa na CBC yenyewe, haukubaini chochote!

Kwa maneno mengine, hakukuwa na sababu kwa yale waliyoyafanya.

Kuna ukosefu mkubwa wa uwazi ndani ya CBC. Maamuzi haya ya kubatilisha leseni ya FBME yamefanywa bila kutilia maanani maslahi ya wafanyakazi zaidi ya 250 – zaidi ya 350 tangia mwanzo wa sakata hili. Kwa kutengeneza madai yasiyo na msingi, CBC imeharibu maisha ya wafanyakazi na kudhoofisha familia hizi.

Je, watu hawa walikuwa na hatia? Wamefanya nini hadi kustahili pigo hili kubwa na familia zao?

Tuseme nini kuhusu wale wote waliopo kwenye taasisi za fedha za ndani na nje ya nchi ambao wanashughulika na FBME? Je, nao wana hatia pia? Biashara ya FBME ya kukutana na wateja moja kwa moja ilikuwa ndogo sana, hivyo miamala mingi ilihusisha benki na taasisi nyingi za fedha ambazo zote zina taratibu zao za kuaminika na viwango bora vinavyozingatia sheria za kimataifa. Je, ni sahihi kwa CBC kutumia ushahidi wake wa uongo kuziadhibu taasisi hizi pia?

Kuna maelfu ya wateja wa FBME na wote hawa wameathiriwa na shutuma za CBC, kwa kukiuka taratibu za kimataifa kama mdhibiti wa nchi. Wote wameathirika vibaya kwa vitendo vya CBC kwa kipindi cha miezi 17. Je, na wao wana hatia?

Hapana, ni wazi kwamba wenye hatia ni kikundi kidogo cha viongozi wa CBC na baadhi ya watu wachache walio nje ya taasisi. Kuna mashaka flani kwamba walikuwa na taarifa ya hatua ya awali iliyochukuliwa na wakala wa serikali ya Marekani – FinCEN dhidi ya FBME na pengine ilishirikiana katika maandalizi yao.

Walichotaka Kukipata ni Nini??

Sasa kwa kuwa mahakama ya Marekani imehoji maamuzi ya FinCEN na kuamuru kwamba maamuzi yao yachunguzwe tena, CBC imevuliwa nguo. Maswali yatatakiwa kujibiwa; mikononi ya watu iliyochafuliwa kwenye mchakato huu itawekwa wazi.

Vile vile, uamuzi wa mahakama ya usuluhishi wa kimataifa ya ICC mjini Paris kufikiria madai ya washitaki, wamiliki wa FBME, kuhusu madhara na fidia dhidi ya Jamhuri ya Cyprus, imeleta pigo zaidi kwa wale waliotengeneza sakata hili kuanzia mwanzo. Madai ya fedha zitaelekezwa kwa Jamhuri ya Cyprus, na walipa kodi wa nchi hii na wawakilishi wao wa kuchaguliwa watataka kujua ni nani aliyesababisha madhara haya.

Kikundi hiki kidogo ndani ya CBC, kinachosaidiwa na baadhi ya watu wa nje ambao waliamini watafaidika, ndio wenye hatia. Ukizingatia kwamba kwa sasa mahakama inawageukia, wanatafuta njia ya kujinasua kutoka kwenye kibano.