Uamuzi wa Mahakama ya Utawala Waonekana Kutokuwa Sahihi

Mei 27, 2016

Maamuzi ya Mahakama ya Kiutawala ya Cyprus kukataa maombi ya Benki ya FBME kuahirisha hatua iliyopangwa ya Benki Kuu ya Cyprus ya kufuta leseni ya tawi ka FBME imetangazwa kuwa hayana mashiko. Maombi ya awali yalifanywa takriban miezi 21 iliyopita kwenye Mahakama Kuu ya Cyprus, na yalikuwa ni maombi kwa ajili ya hukumu ya mpito. Mahakama ya Utawala iliisikiliza kesi hiyo ili kupunguza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama Kuu, na inajulikana kwamba Mahakama ya Utawala haina kawaida ya kutoa maamuzi ya mpito.

Maamuzi halisi ya kesi zilizopo kwenye mahakama za Cyprus na Marekani, na mahakama ya usuluhishi ya Ufaransa yatafanywa katika miezi ijayo. Kwa mfano, mwanzoni mwa mwezi Juni kutakuwa na usikilizwaji wa kesi kwenye mahakama ya Wilaya ya Washington DC kuhusu vitendo vya FinCEN, ambayo ilisababisha uamuzi wa CBC kuiendesha benki ya FBME tawi la Cyprus kupitia matumizi mabovu ya Sheria ya Azimio. Matokeo ya kesi hii yanaweza kuwa na athari kubwa kwa kesi inayoendelea kisheria nchini Cyprus na mahali pengine.