Ombi la CBC la Kutaka Maelezo Binafsi ni Kinyume cha Sheria

Mei 24, 2016

Mawasiliano ya hivi karibuni kutoka Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kwenda kwa wamiliki wa akaunti wa tawi la Benki ya FBME Cyprus ni kinyume cha sheria na inapingana na maamuzi yoyote ya kisheria ya huko nyuma, FBME imesema. Mawasiliano hayo, yaliyoitwa na CBC “maelezo ya mwenye akaunti ‘”, yanawataka wamiliki wa akaunti kuwasilisha maelezo yao binafsi na ni mbinu ya mlango wa nyuma ya kuwafanya waombe malipo ya dhamana ya amana bila ya wao kujua.

Ikishajazwa na kurudishwa taarifa hii itafuta haki zote za amana iliyo juu ya ukomo wa CBC ya Mfuko wa Dhamana ya EUR 100,000 – hata kama ni wazi kwamba FBME ina fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya wateja wote. Aidha, itakuwa na maana kwamba wateja watapoteza haki yao ya kuchukua hatua za baadaye dhidi ya CBC kwa uzembe wake na uendeshaji wa hovyo wa Benki ya FBME.

Vipengele muhimu kwenye fomu ya CBC ni vya 12, 13 na 14:

12. Mtu anayesaini fomu hii anaikabidhi mamlaka ya mfuko wa dhamana – DGS haki zake, umiliki na maslahi yoyote aliyonayo kwenye Benki ya FBME tawi la Cyprus hadi kufikia kiasi kinacholipwa na kwa wakati kiasi hicho kitakapolipwa na DGS.

13. Bila ya kuathiri kipengele cha 12, mtu anayesaini fomu hii anafungwa nayo na hatakuwa na haki yoyote ya kupigania haki au maslahi yake kwa akaunti anazomiliki katika benki ya FBME tawi la Cyprus hadi hapo DGS itakapopata fedha za malipo kutoka Benki ya FBME tawi la Cyprus. Katika kipindi hiki, mtu anayesaini fomu hii atahamishia kwenye DGS kama itakavyoagizwa na DGS, kiasi chote kitakachowekwa na mtu mwingine tofauti na DGS kuhusiana na akaunti inayomilikiwa na mtu anayesaini fomu kwenye Benki ya FBME tawi la Cyprus.

14. Mtu anayesaini fomu hii anaiteua bila kipingamizi DGS kuwa wakili wake kwa madhumuni ya kumwakilisha kwenye mambo yote ya kuamua, kusaini na, kama inahitajika, kusajili kwa niaba yake nyaraka zozote ambapo mtu anayesaini fomu hii angeweza kufanya kwa mawasiliano; kuamua, kusaini au kusajili ili kutekeleza kikamilifu kipengele cha 12 na 13 hapo juu.

Kama tulivyothibitisha mwezi mmoja uliopita, wateja 300 tu ndio walioomba kwa CBC malipo kutoka kwenye mfuko wa dhamana. Hii ni nje ya wamiliki 6,500 wa akaunti waliopo FBME tawi la Cyprus. Inawezekana tu kubashiri juu ya nia ya wateja 120 ambao wamefanya hivyo, lakini kuna uwezekano kwamba wengi watakuwa wateja na makampuni walio na salio la EUR 100,000 au chini.

Ni vema kuwakumbusha wasomaji kwamba malipo yoyote kwenye mpango wa CBC yanapaswa kutoka kwenye mfuko maalum na tofauti uliopo benki kuu ambapo benki zote za Cyprus wamekuwa wakilipwa katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo nia ya CBC, iliyo wazi kabisa, ni kutumia fedha za wateja wa FBME kulipia fidia za bima zao, kwa kukiuka sheria husika za Cyprus na EU.