Uchunguzi wa Marekani unaendelea Benki ya FBME

Agosti 7, 2014

Wataalamu wa uchunguzi wa kihasibu wali wasili Cyprus siku ya Jumatano, Julai 30 kuanza uchunguzi kuona kama taratibu za kugundua fedha chafu za Benki ya FBME zipo sawa. Uchunguzi ni sehemu ya ushiriki wa Benki kwa Idara ya Hazina ya Marekani kufuatia tangazo la FinCEN la ilani ya uchunguzi na matokeo ya tarehe 15 Julai 2014.

FBME itakuwa ikikabiliana na masuala yaliyozungumzwa katika matangazo haya, ambayo imesababisha kuwaagiza kufanya uchunguzi huu wa kujitegemea. Benki inaahidi kufuata taratibu za kupambana na pesa chafu kwenye mpango wake na inathibitisha dhamira yake ya kutatua masuala yaliyojitokeza katika Ilani zote hadi hapo FinCEN itakaporidhika.

Wanahisa wa FBME wanasema kwamba uchunguzi utakuwa ni wa uhakika na wenye ushirikiano. Kazi hii itahusisha na kuona kama Benki inafuata taratibu za EU za kuzuia fedha chafu na kanuni ya Jua Wateja Wako na miongozo bora kibenki.

Aidha, Benki imemteua mshauri wa nje katika jiji la Washington katika kuhusiana na masuala yaliyotolewa na Marekani Idara ya Hazina. Wanahisa wa FBME Benki wametoa wito wa muda wa kutosha kuruhusiwa kwa ajili ya uchunguzi kushughulikia masuala yaliyotolewa na idara ya Hazina ya Marekani. Wakati huo huo, Benki Kuu ya Cyprus ilianza uchunguzi mpya tawi la FBME Cyprus, sambamba na kanuni za kawaida za udhibiti. Hii inafuatia uchunguzi hivi karibuni katika sekta ya fedha jijini Cyprus ikiwa ni pamoja na FBME, uliofanywa kwa niaba ya Benki Kuu na kampuni ya kimataifa ya ushauri, PwC, kati ya tarehe 17 Juni na Julai 4, 2014. Ripoti imeandika kuwa matokeo ya uchunguzi huu hayajatolewa kwa FBME wala wanahisa wake , lakini katika mazungumzo na viongozi wa Benki Kuu imewekwa wazi kwamba ukaguzi hauku gundua matokeo yeyote mazito ya fedha chafu.

Wanahisa wa FBME waliongeza kuwa msimamo wa Benki kifedha ni mzuri na mkamilifu na uko sambamba na mtaji toshelevu na solvens yanayohitajika na Benki Kuu ya Ulaya. Wakati wa kutangazwa na idara ya Hazina, uwiano wa muda mfupi wake ukwasi, ulikuwa katika 104%, kuweza kutosha kufidia amana zote.