Juni 10, 2015
Wakati mvutano ukiendelea kuhusu utendaji wa viongozi waandamizi wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC), imependekezwa kwa mara nyingine tena kwamba taasisi hii lazima iwapime wakurugenzi wake na uongozi mzima.
Duru ya hivi karibuni ya utata unaowakabili viongozi waandamizi wa CBC unawekwa vizuri kwenye kumbukumbu na vyombo vya habari nchini Cyprus. Kashfa mpya ni karibu matukio ya kila siku na CBC ipo kwenye mgogoro mkubwa. Gavana mwenyewe anakabiliwa na kamati ya kimahakama ya Bunge kuhusu mwenendo wake na inapelekea hadi kujiuliza swali kubwa kuhusu uwezo wa viongozi wa CBC kufanya kazi. Haya yanafuatia ripoti mbaya juu ya CBC iliyotolewa wakati na baada ya kuanguka kwa Sekta ya Benki nchini Cyprus mwaka 2012 na 2013 ambapo msimamizi alionekana kushindwa kuimudu na hatimaye kuanguka kwa Sekta ya Benki Cyprus.
Ni vema tukajikumbusha kwamba hakuna mjumbe hata mmoja wa Bodi ya Wakurugenzi wa CBC aliyewahi kufanya kazi katika benki. Mmoja tu, George Syrichas, aliyewahi kufanya kazi CBC – na yeye ni mchumi. Gavana ni mfanyakazi wa muda mrefu katika utumishi wa umma na kupanda hadi kuwa Mkaguzi Mkuu kabla ya kuteuliwa kama Gavana wa CBC, lakini haikufanyika kwa kuzingatia kufaulu mtihani wa Benki au mtihani wa usimamizi wa Benki.
Mameneja waandamizi katika CBC ni wahasibu na ingawa hakuna shaka wa uwezo katika maeneo hayo hakuna aliyefanya kazi benki au kufaulu mtihani wowote kuhusiana na masuala ya benki au jukumu la mamlaka ya usimamizi. Wengi wa watu hawa walilaumiwa mno na vyombo vya kimataifa vilipochunguza nini kilichotokea wakati wa mgogoro wa benki nchini Cyprus. Wakati hakuna pendekezo la kuwashirikisha na mgogoro wa sasa wa CBC lakini kuna marejeo mengi yanayoonyesha kuwepo kwa upungufu wa utaalamu. kwenye usimamizi
Ukosefu huu wa ujuzi wa mifumo ya benki inaweza kuwa sababu ya maafisa hawa waandamizi kulazimisha hatua ya Azimio kwa FBME tawi la Cyprus Julai iliyopita, siku mbili tu baada ya tangazo la FinCEN juu ya Matokeo na Mapendekezo yakuchukuliwa. Azimio hilo lilikuwa sio njia sahihi na pengine lilikuwa si la kisheria kwani lilianzishwa kwa ajili ya benki inayofilisika, na sio iliyo na afya kifedha kama FBME.
Kukosekana huku kwa uelewa juu ya jukumu la CBC kunaweza kukawa kumechangia hadi kwenye Azimio la FinCEN. Badala ya kuilinda benki iliyopo katika eneo lake la usimamizi, CBC ilionekana kuchochea mashambulizi yake. Badala ya kupanga mbinu za pamoja na mamlaka ya Msimamizi mkuu wa FBME, Benki Kuu ya Tanzania, iliwapuuza na kufanya maamuzi peke yake. Kwa kweli, ilionyesha tabia mbaya na kukiuka miongozo yote ya kimataifa.
Na badala ya kufuata miongozo ya Basel na Benki ya Ulaya ambayo imewekwa kwa ajili ya benki kuu kushughulika na taasisi katika utatuzi wa migogoro, yote hii iliipuuza. Kwa kweli, maofisa waandamizi wa CBC ambao walishughulika na tatizo la FBME tawi la Cyprus walionekana kabisa kutojali kuwepo kwa miongozo. Kama tujuavyo, wale waliofanya hayo – Gavana na Wakurugenzi wake waandamizi wawili (wanaounda Kamati ya Azimio), mmoja akiwa Mkuu wa Kitengo cha azimio, Michalis Styllianou – alifanya hivyo bila ushauri wa Mamlaka ya Azimio, chombo cha juu katika suala hilo. Hivyo, mbali na kuvunja kanuni za kimataifa, walivunja pia kanuni zao wenyewe nchini Cyprus.
Kama tujuavyo, matokeo ya mambo yote haya yanaweza kuifanya Jamhuri kukumbwa na madai ya fidia ya mamia ya mamilioni ya Euro. Tusichokijua – kwa sababu ya ukosefu wa uwazi kamili unaohusishwa na vitendo vya viongozi hawa waandamizi – ndio sababu walifanya na kupata matunda waliotarajia. Hawajaongelea kuhusu nia yao, mbali na maoni ya baadhi yao kuhusu kulinda wateja, watu ambao wamewaumiza sana, na ya kuuza tawi, kitu ambacho hawawezi kukifanya.
Hivyo kama hawaongei wanawakaribisha wengine kuwaongelea, na hivyo kusababisha kufikiriwa vibaya kwa matendo yao.
Ni wakati muafaka kwa Cyprus kufikiria tena juu ya maoni yetu ya awali kwamba wekurugenzi waandamizi wa CBC na maafisa wengine wapimwe kwa kutumia vipimo sahihi vinavyotakiwa kwa kabla ya uteuzi wao na wanapopewa nafasi mpya.
Vipimo hivi lazima kuchunguza ujuzi wa kazi zao na masuala mapana ya benki na fedha, pamoja na viwango vya kuangalia tabia na mitazamo yao. Vipimo ni lazima vihusishwe na kuhudhuria kozi ya lazima na kufaulu mitihani.
Majanga ya miaka ya hivi karibuni yanamaanisha ni vigumu kwa Jamhuri kuendelea bila kupitisha mfumo kama huu. Tatizo ni kwamba bila viwango vya juu vya udhibiti mkubwa, matatizo ya siku za nyuma daima yatajirudia. Kusiwe na uteuzi wa kisiasa kwenye eneo hili muhimu na mtazamo mpya kabisa kufuatwa wakati wa kuwapa watu nafasi za juu.
Kama mabenki yanapata vipimo hivyo basi hata Benki Kuu ni lazima wapimwe.
Kama tulivyosema hapo awali, kila mkurugenzi na meneja mwandamizi wa Benki ya FBME tawi la Cyprus na kwenye Kitengo cha Kadi wote wamepitia vipimo hivyo.