Aprili 12, 2016
Wafanyakazi wa Benki ya FBME nchini Cyprus wameanza mgomo hadi itakapotangazwa tena. Wamegoma kwa sababu ya matendo ya hovyo ya Msimamizi Maalum ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC), pamoja tabia na matendo ya CBC na Mamlaka za Cyprus kwa ujumla. Kauli imetolewa na wafanyakazi ambayo inasomeka kama ifuatavyo:
“Sisi, wafanyakazi wa Benki ya FBME, kuanzia leo 11 Aprili, 2016 tunaingia kwenye mgomo / maandamano kwa sababu ya uvunjwaji wa haki zetu kama wafanyakazi. Baada ya takriban miaka miwili ya kuwa chini ya utawala wa Benki Kuu ya Cyprus tumechoka na tabia mbaya na udhalilishaji kwa wafanyakazi.
Katika kilele cha tabia hii siku chache zilizopita wenzetu wawili walifukuzwa kinyume cha sheria na kwa uonevu, kwa sababu tu walithubutu kueleza matatizo ya makosa anayofanya Msimamizi Maalum wa tawi la FBME Cyprus, Bw Chris Iacovides, na Benki Kuu walipotutaka sisi wafanyakazi, kupeleka kwa wateja wa Benki ya FBME taarifa za uongo zinazohusiana na ma/salio ya akaunti zao.
Siku mbili baadaye, wakati wafanyakazi tukijiandaa kuchukua hatua kwa kitendo batili walichotendewa wenzetu hao wawili, wafantakazi 136 kati ya 165 walipokea barua za kusitishiwa ajira, ikiwa ni pamoja na wanawake wajawazito 8 na akina mama wenye likizo ya uzazi! Hadi leo wafanyakazi walioachishwa hawajapata ilani ya kisheria ya kuachishwa ajira kama sheria inavyosema, sehemu ya likizo yao ya kila mwaka na mafao yao mengine waliyoyafanyia kazi. Haya ni mafao yanayolindwa na sheria, ambayo yamechumwa kufuatia miaka mingi ya kufanya kazi na kama yasipolipwa yanapelekea uvunjwaji wa haki za kimsingi za ajira.
Dk Pavlos Kourtellos, mshauri wa sheria wa Msimamizi Maalum, anashikilia msimamo wake kwamba barua zilizokabidhiwa kwa wafanyakazi waliosimamishwa na Msimamizi Maalum sio za kufukuzwa wala kupunguzwa kazi, bali “kukatisha” mkataba na anasema kwa sababu ya “kukatishwa” huko kwa mkataba hatustahili malipo ya ilani, likizo zilizosalia, sehemu ya mshahara wa 13, na marupurupu mengine. Melezo haya ya kisheria hayakubaliki na kundi lolote la wanasheria, kwani hayapo kwenye sheria za kazi. Mtu pekee anayeonekana kuyakubali ni Mr Iacovides, kwani yanaisaidia agenda yake, ambayo ni kupunguza gharama ya Benki kwa kutolipa wafanyakazi, ili kuifanya Benki Kuu iwe na fedha nyingi zaidi kuwalipa wadai. Hata hivyo, kila wakati wanapoongelea juu ya kufukuzwa kazi wanajikuta wanasema kuachishwa kazi… Huu ni utata unaofurahisha
Kitu ambacho Dr Kourtellos hajamueleza Mr Iacovides, ni kwamba kwa kufuata msimamo huu, ufukuzaji wa wanyakazi unakosa nguvu ya kisheria, ambao unaweza kusababisha wafanyakazi kuwa na haki ya madai ya usumbufu yenye thamani ya mamilioni ya Euro, ambayo kama benki ikifilisiwa yatatakiwa kulipwa na mfuko wa ‘uachishaji kazi’ (Redundancy), kwa maneno mengine Serikali!
Ni lazima ieleweke kwamba wafanyakazi waliobaki wanakabiliwa na matatizo makubwa katika kutekeleza majukumu yao kwa usahihi. Kwa upande mmoja ni kutokana na kuachishwa kazi kwa wenzetu 136, ambapo imeacha nafasi muhimu bila watu; na kwa upande mwingine kutokuwa na uhakika wa mafao yetu, ambayo yalikuwa yakitambuliwa na mwajiri wetu (Benki) kama malipo halali pamoja na wasimamizi wawili waliopita.
Idadi kubwa ya wafanyakazi wanapata mshahara wa wastani. Watu wenye familia, ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaotegemewa na familia zao. Uhitaji wa mshahara unatumika na Msimamizi Maalum kama chombo cha majadiliano katika misingi ya aibu na udhalilishaji. Waliwafuata wafanyakazi wenzetu walioachishwa kazi ili kuwaajiri tena kwa mshahara kama wa zamani ukitoa wiki ambazo waligoma. Aidha, Msimamizi Maalum amesema kuwa atazuia malipo ya kipindi cha ilani mpaka hapo tabia na kiwango cha ushirikiano na wafanyakazi waliobaki kitaboreka.
Benki Kuu haitaki kumwajibisha Msimamizi Maalum waliomteua kwa kuvunja sheria, hata kama anazuia fedha ambazo zingeweza kutumika kulipa mafao ya wafanyakazi na badala yake kuamua kumpa majukumu Mr Iacovides. Sheria ya kazi imekiukwa kabisa dhidi ya wafanyakazi wote.
Sisi wafanyakazi tunaona wote wawili wanawajibika.
Tunachohitaji sisi ni malipo yetu ya msingi.
Tunahitaji:
- Kuondolewa mara moja uachishwaji kazi haramu
- Malipo ya haki zetu kamili kwa haraka
- Kutendewa haki
- Kuheshimu sheria kwa ulinzi wa akina mama na wajibu kwa akina mama
Madai yetu yote yanalindwa na sheria na tutaendelea kugoma hadi hapo tutakapotimiziwa.”