Uamuzi wa CBC ni Kinyume cha Sheria na Usiofaa

6 Aprili 2016

Msimamizi Maalum wa Benki ya FBME tawi la Cyprus ametoa barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi 136 ili kupunguza gharama na kulinda amana. Sababu alizotoa eti ni kubana matumizi na kulinda amana za wateja?! Hivi sasa Benki ina mtaji na akiba ya dola milioni 162 zaidi ya fedha zinazohitajika kufidia amana zote na gharama yoyote itakatwa kutoka kwenye fedha hizi. Pamoja na hayo, sababu inayosemekana kubana matumizi haina maana yoyote kwa wateja. Hakika, kinyume chake, uwezo wa benki wa kuhifadhi mali zake umeathiriwa vibaya kwa sababu ya kuwapoteza wafanyakazi hawa.

Hatua hii haina maana na imechukuliwa kinyume cha sheria; Msimamizi Maalum sio mwajiri wa wafanyakazi wa Benki ya FBME na yeye hana uwezo wa kusitisha mikataba ya ajira. Uharamu huu unatokana na kukataa kuwalipa wafanyakazi haki zao halali. Hata hivyo, kuondolewa kwa wafanyakazi hao kunaliacha tawi la Cyprus na wafanyakazi wachache kiasi kwamba sio tu hawataweza kutoa huduma za kawaida, bali pia hawataweza kuendesha zoezi haramu la kufilisi tawi hilo lililopendekezwa na Benki Kuu ya Cyprus (“CBC”).

Sambamba na hili, Msimamizi Maalum anataka kuwaandikia wateja wote kuwataka kuthibitisha amana zao za sasa katika Tawi la FBME Cyprus. Tangu leseni ya tawi isitishwe na CBC shughuli za kibenki zimekoma matokeo yake mifumo ya kompyuta haiwezi kuhuisha salio/amana kihalali na mihutasari ya akaunti haijachapwa. Kwa maana hiyo, mpango uliopendekezwa unaoshirikisha kutoa taarifa zisizo sahihi kwa wateja huku wakijua sio sahihi, na kuwataka wateja wathibitishe taarifa zisizo sahihi inaweza kusababisha vitendo vya udanganyifu.

Vitendo hivi vya CBC ni jaribio la wazi kabisa la kufikia azma yake haramu ambayo wameshindwa kuifikia kupitia kwenye mahakama. Lengo ni kuizuia Benki ya FBME kudai haki yake ya kisheria nchini Marekani na Cyprus. Hatua hii ni potofu na pia ni kinyume cha sheria; italeta dhima hasi ya CBC kwa wateja wa Benki ya FBME na pia inaongeza dhima hasi ya Jamhuri ya Cyprus kwa wamiliki wa Benki ya FBME. Hatimaye itakuwa ni wateja wa benki, wafanyakazi na walipa kodi watakaoathirika asante kwa CBC kwa kuendelea na ubishi wa kutotaka kufuata sheria au mawazo mema.