Msimamizi Afikia Kiwango Kipya

Desemba 31, 2014

Kiwango cha malipo ya kila siku kimepunguzwa hadi EUR 1,000 kwa siku, kulingana na amri iliyotolewa na Msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus, Dinos Christofides. Kwa nini amepunguza kiwango – kilichowekwa mwanzoni EUR10,000, kisha kikawa EUR 5,000 hivi karibuni kufikia EUR 2,000 – hajaamua kushirikiana nasi. Kuna mamilioni ya Euro yaliyopo katika Benki Kuu ya Cyprus (ambayo FBME inaendelea kulipa adhabu) na hakuna hatari ya benki kuwa mufilisi. Ni nini haswa malengo yake?

Uamuzi wa awali wa kuweka kiwango cha juu ulikuwa ni kosa kubwa kama alikuwa na nia ya kujenga mahusiano mazuri kati ya wateja na Benki ya FBME tawi la Cyprus. Hii inajenga hali ya kuilazimisha Benki ifilisiwe. Kubadilisha viwango anaifanya hali iwe mbaya.  Kutotaka kwake kutoa maelezo au sababu, msimamizi anaonekana kufanya maamuzi ya ghafla yanayo athiri maslahi ya wateja. Kwa sasa tunaamini kwamba maslahi ya watu 100,000 yameathiriwa moja kwa moja na maamuzi haya, na kuthihirisha uongo kuwa sera ya Benki Kuu ya Cyprus tangu mwanzoni mwa tukio hili ni “kulinda maslahi ya wateja”. Nia hiyo inaonekana kuchomokea dirishani kama kweli ilikuwa na udhati tangia mwanzo.
Ingeeleweka zaidi kama Benki Kuu ya Cyprus, chombo kilichoundwa kusimamia masuala ya benki na matawi ya benki katika Jamhuri, ingeweza kujibu maswali kuhusu matendo na nia yake. Tuliweka idadi ya maswali ya kuridhisha katika tovuti hii tarehe 31 Oktoba na kabla ya hapo, tarehe 10 Septemba. Katika nchi nyingine, vyombo vya serikali, hata kikiwa kikubwa kama Benki Kuu, vinawajibishwa. Hapa, inaonekana wasimamizi wa benki wa kicyprus, wanahisi wao ni zaidi ya masuala haya. Kwa sababu sasa wanakabiliwa na kesi kwenye mamlaka ya kimataifa ya ICC, labda watakuwa na cha kusema.