Author Archives: Editor1

Maendeleo ya Kesi ya Benki ya FBME

Septemba 18, 2014

Tarehe 17 Julai, FinCEN alitangaza Taarifa ya Matokeo na Mapendekezo dhidi ya FBME Bank. Amri hiyi illitaka FBME iwasilishe majibu yake ya umma ifikapo tarehe 22 Septemba. Kampuni ya sheria ya kimataifa ya Hogan Lovells ilitakiwa kuwasiliana na FinCEN na kwa upande mwingine kushirikiana na wataalam wa Enst and Young kufanya uchunguzi huru kuhusiana na mifumo na sera za Kupambana na Fedha chafu ndani ya FBME na kuona kama mifumo na sera hizo zinalingana na mamlaka za Benki Kuu ya Cyprus na zile za Umoja wa Ulaya.

Continue reading

Mahakama yaahirisha Kusikiliza Kesi ya Uuzaji

Septemba 16 2014

 Mahakama ya Wilayaya Nicosia jana iliahirisha kesi ambayo iliwasilishwa na wamiliki wa FBME ya kusimamisha uuzaji wa Benki kwa sababu faili la kesi hiyo liliwasilishwa mahakamani wakati huo. Ilifahamika pia kwamba serikali ya Cypus ambayo ni mshitakiwa kwenye kesi hii, walishindwa kuwasilisha utetezi wao kwenye muda ulipangwa. Masuala ya utaratibu yalizingatiwa na Mahakama imelipanga shauri hili kufanyika tarehe 29 Octoba, 2014. Benki kuu imerejea ahadi yake ya kutotekeleza Azimio lolote aukuingia mkataba wowote kuhusiana na uuzaji wa tawi la Benki hadi hapo hukumu ya shauri hili itakapotolewa.