Maendeleo ya Kesi ya Benki ya FBME

Septemba 18, 2014

Tarehe 17 Julai, FinCEN alitangaza Taarifa ya Matokeo na Mapendekezo dhidi ya FBME Bank. Amri hiyi illitaka FBME iwasilishe majibu yake ya umma ifikapo tarehe 22 Septemba. Kampuni ya sheria ya kimataifa ya Hogan Lovells ilitakiwa kuwasiliana na FinCEN na kwa upande mwingine kushirikiana na wataalam wa Enst and Young kufanya uchunguzi huru kuhusiana na mifumo na sera za Kupambana na Fedha chafu ndani ya FBME na kuona kama mifumo na sera hizo zinalingana na mamlaka za Benki Kuu ya Cyprus na zile za Umoja wa Ulaya.

Ilipofika saa 5 usiku wa tarehe 21 Julai Benki Kuu ya Cyprus ilitangaza kuiweka benki ya FBME tawi la Cyprus chini ya udhibiti wake – Benki ambayo ilikuwa na fedha za kutosha . Sheria hii iliwekwa ili kuzishughulikia Kampuni ambazo hazina Fedha. Hili lilifanywa bila kushirikisha  benki Kuu ya tanzania ambayo ndio mdhibiti mkuu wa Benki ya FBME matokeo yake mamlaka za Tanzania zilimteua Meneja mdhibiti ili kuendesha shughuli za FBME benki za makao Makuu, matawi yaliyopo Tanzania na kuangalia uendeshaji wa tawi la Cyprus. Juhudi zote za Meneja Mdhibiti za kufanya kazi kwa karibu na Benki Kuu ya Cyprus zilishindikana baada ya kutopewa ushirikiano na mamlaka za Cyprus.

Benki Kuu ya Cyprus ilimteua Dinos Christofides kuwa Msimamizi maalum wa tawi la Cyprus tarehe 22 Julai. Alitangaza kuwa nia yake ilikuwa ni kuuza tawi, tena bila kumshirikisha Meneja mdhibiti  wa Benki au hata wamiliki wa FBME. Bwana  Christofides alikuwa na uhusiano na Kampuni ya Kifedha la Sweden ambayo ilitangaza nia yake ya kupata leseni ya benki nchini Cyprus. Baada ya kugundulika mgongao wa Kimaslahi, bwana Christofides alijiuzulu  kutoka kwenye nafasi yake na kampuni hiyo kwa barua ya tarehe 31 Julai iliyokuwa na tarehe ya nyuma.

Hakuna wakati wowote Mr Christofides aliwasiliana na wamiliki wa Benki wakati anataka kuuza Benki hii, ambao walianzisha kampeni ya kisheria kupinga uamuzi huo uliojulikana kama uvamizi baridi. Wachambuzi wa mambo wameelezea hatua ya Benki Kuu ya Cyprus kuwa ‘ isiyo “Utaifishaji” na wamehoji nia na mazoea ya mamlaka za Cyprus.

Tarehe 30 Julai, wanasheria wa kimataifa na wahasibu wachunguzi waliwasili Cyprus kutathmini kwa kina mifumo na sera za benki ya FBME za kupambana na fedha chafu na kufanya miamala ya majaribio ili na hatimaye kujibu tuhuma zilizotolewa na FinCEN. Wataalam hao walikataliwa kuingia ndani ya jengo la FBME na Msimamizi Maalum bwana  Christofides, bila ya maelezo yoyote, uamuzi ambao CBC iliupindua baada ya kupata ushauri toka Mahakama Kuu.

Uendeshaji wa Benki ya FBME tawi la Cyprus ulisimamishwa kwa Azimio la Amri lililotolewa tarehe 23, 24, 25 na 28 Julai. Tawi ilibidi lifunguliwe kama sheria inavyoagiza, lakini kwa kweli shughuli za uendeshaji zilikataliwa na Msimamizi. Hivyo, kinyume na barua ya sheria, tawi lilibakia limefungwa. Msimamizi alidai hii ni kutokana na kukataliwa na Mabenki Mwambata (Correspondence Banks) kufanya biashara na FBME ingawaje utawala wa Benki uliwashauri kwamba kuna Benki zilizokuwa tayari kufanya Biashara ya Uambata na FBME.

Pamoja na jitihada za mara kwa mara kupata taarifa ya maandishi toka kwa msimamizi ili wateja na umma zwatambue na kushauriwa kuhusu nini kinachotokea, alichoruhusu yeye mambo machache aliyotolea maamuzi kwa maneno tu. Kwa kuona madahara yanayosababishwa na matatizo haya ya mawasiliano kwa benki na wateja wake, wanahisa wa FBME walianzisha kampeni zao wenyewe za mawasiliano.

Kwa kutoweza kupata fedha za kufanyia malipo wafanyabiashara wa kadi, FBME ililazimika kusitisha huduma za kitengo cha kadi tarehe 7 Agosti. Pamoja na maombi kwa Msimamizi kutoa fedha kwa Kitengo cha huduma za Kadi ili kuendelea kufanya kazi, msimamizi alikataa maombi yote na kusababisha kupunguzwa kwa wafanyakazi 72 wa kitengo kilichokuwa kikifanya biashara vizuri

On Agosti 18, Msimamizi aliamuru Benki Mwambata wa FBME kuhamisha amana za wateja kwenda kwenye akauti mojawapo ya Benki Kuu ya Cyprus. Hatua hii ilizuiwa na Meneja Mdhibiti wa Tanzania ambaye aliamuru kusitishwa kwa mfumo wa SWIFT. Hakuna maelezo yaliyotolewa na msimamizi wa Nicosia kwa hatua hii, ni vema pia kujua kwamba Benki Kuu ya Cyprus hadi sasa anashikilia zaidi ya milioni Euro 100 za amana za FBME.

Tarehe 1 Septemba, Msimamizi alitangaza kuwa baadhi ya wateja wangeweza kupata fedha zao nchini Cyprus kwa kiasi cha EUR10,000 kwa siku, wakati wateja wengine bado akaunti zao zilikuwa zimefungwa.

Wale ambao waliruhusiwa kupata fedha zao walilazimika kupata kitabu cha hundi na kufungua akaunti katika Benki ya Cyprus. Nusu-hatua hii, ilisababishwa na malalamiko yaliyopokelewa na Benki Kuu na bado wateja waliokuwa nje ya Cyprus walinyimwa huduma ingawaje wote wako kwenye hadhi inayolingana.

Kwa uchungu wa malalamiko dhidi yake kwa matendo yake yanayosababisha madhara makubwa kwa wateja na biashara kwa Cyprus na nje ya nchi, Msimamizi ametoa vitisho kwa wafanyakazi wa FBME, ikiwa ni pamoja na kutaka kuzuia malipo na mishahara. Kuna ushahidi wa madahra uliofanywa, pia, kwa sifa ya Cyprus kama kituo cha biashara kutokana na vitendo vyake.

Septemba 5, tovuti ya wanahisa ya fbmeltd.com ilisizuiwa kwa kile kinachoonekana kuwa ni Unyimwaji wa huduma mkubwa kwa ‘udukuzi’ unaofanyika. Ndani ya masaa 24 tovuti iliweza kupatikana na kuhamishiwa nje ya Jamhuri ya Cyprus.

Usikilizaji wa kesi kwenye Mahakama ya Wilaya ya Nicosia ya wito wa kusimamisha maamuzi ya mauzo ya tawi la Benki ya FBME Cyprus yaliahirishwa tarehe 15 Septemba wakati Jamhuri ya ya Cyprus aliposhindwa kuwasilisha upinzani wake kwa wakati. Tarehe mpya ni 29 Septemba.

Ripoti ya uchunguzi ya kihasibu imeshatayarishwa tayari kwa ajili ya kuwasilishwa FinCEN.