CBC Yafyeka wafanyakazi136 wa FBME Cyprus

2 Aprili 2016

Chris Iacovides, Msimamizi Maalum ya Benki ya FBME tawi la Cyprus ambaye aliteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) mwezi Januari, amewakabidhi wafanyakazi 136 wa tawi la Cyprus barua za kuwaachisha kazi tarehe 31 Machi 2016, ikiwa ni sehemu kubwa ya wafanyakazi waliobaki Cyprus. 

Katika suala hili, ni lazima ieleweke kwamba CBC imeomba kwenye Mahakama ya Wilaya ya Nicosia kufilisi tawi la Benki la Cyprus pamoja na makao makuu ya benki yaliyopo Tanzania kwa madai kwamba imefilisika. Benki ya FBME inapinga kwa nguvu zote uhalali wa kufilisi tawi na makao yake makuu, ambapo dhumuni pekee la maombi hayo ni kuleta madhara kwa Benki ya FBME kutoka Benki Kuu ya Cyprus (CBC) wakati kesi za kisheria bado zinaendelea katika Mahakama ya wilaya ya Nicosia.

Mnamo Desemba 22, 2015 CBC iliomba kwa siri kwenye mahakama ya Cyprus kufilisi tawi la Benki lakini ilishindwa kuweka jambo hilo kuwa siri kwani liliingiliwa kati na Benki ya FBME mahakamani.

Hii hatua ya karibuni ya CBC na Msimamizi wake ya kuwaachisha kazi wafanyakazi wengi ina nia ya kuleta madhara yale yale bila kufuata misingi ya kisheria. Hatua hii itapingwa vikali mahakamani na Benki ya FBME.

Upunguzaji wa wafanyakazi wengi wa tawi kiasi hiki ni jaribio jingine la CBC la kuzuia tawi kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wateja wake wa muda mrefu. Mpaka sasa, wateja hawa wamekuwa wakihudumiwa na tawi kwa uwazi na kitaalamu kwa mujibu wa kanuni na taratibu zinazotambuliwa za benki.

Mishahara ya wafanyakazi katika Benki ya FBME ilikuwa ikilipwa vizuri kabla ya mwisho wa mwezi. CBC na Msimamizi wake wanaendeleza sera za unyanyasaji na vitisho kwa kusababisha ucheleweshaji wa makusudi na dhiki isiyo ya lazima kwa wafanyakazi wa Benki. Mapema vyombo vya habari vilimsikia msimamizi akisema atashikilia malipo yao maalum ya kustaafu kazi, ambayo ni haki yao chini ya sheria.