Mei 18, 2015
Dinos Christofides, mhasibu aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC), kuiendesha Benki ya FBME tawi la Cyprus ameacha ghafla jukumu lake hilo Ijumaa Mei 15 mwaka 2015. CBC alitangaza kwenye tovuti yake kwamba Mr Christofides amejiuzulu kwa sababu za kibinafsi, ingawa katika mazungumzo mengine alitoa mtazamo tofauti.
Mameneja waandamizi wa FBME waliambiwa kwamba msimamizi wa pili aliyeteuliwa na CBC, Andrew Andronikou, atachukua nafasi yake. Mr Andronikou ni Mwingereza ‘wakala wa kubadilisha na kufufua biashara’ mwenye asili ya Cyprus. Hana uzoefu wa kibenki.
Hivyo inaonekana ni fursa nzuri kwa CBC na msimamizi wake kupata msaada wa kitaalam kutoka kwa wasimamizi waandamizi wa FBME na Bodi ya Wakurugenzi kuboresha uendeshaji wa tawi kwa faida ya “Wateja na wadau wengine”. Isitoshe, tawi la FBME nchini Cyprus limekuwa na historia ya miaka 33 wakati ambapo limekuwa moja ya matawi yenye nguvu katika soko la ndani la benki kabla ya kuwekwa chini ya Azimio. Kama CBC ipo makini kuhusu kupunguza madhara na kukomesha fidia zijazo kwa gharama za walipa kodi, sasa ni wakati muafaka.
Msimamizi mpya wa CBC anatakiwa kuchukua maoni ya wasimamizi wa FBME kwenye barua iliyoandikwa kwa Dinos Christofides tarehe 2 na Machi 13 2015. Barua hii ilikuwa yenye heshima sana ingawa ilizungumzia ‘ukosefu wa mkakati mahsusi kutoka kwa Mr Christofides na pia kutokuwa na mawasiliano kabisa kati yake na uongozi juu ya mpango mkakati wa tawi. Barua ya Machi 2 ilihusisha ombi la kusaidia katika kuyatimiza maslahi muhimu ya wateja. Baada ya majibu kutopatikana, ilitumwa barua ya pili siku 11 baadaye kuomba kutoa msaada kwa wasimamizi kuwa kama “kichocheo katika kutambua majukumu yajayo, na kuongeza: “Tunaamini unatambua lengo letu, yaani kutunza maslahi ya wateja’, utulivu wa mfumo wa fedha na matokeo mema ya Benki na Tawi lake “.
Hatimaye jibu kutoka kwa Mr Christofides liliibuka tarehe 15 Aprili 2015, ambapo “alikataa madai yote yaliyotolewa katika barua hiyo”, na kukataa maoni zaidi kwani suala hilo lilikuwa mbele ya mahakama. Kwake yeye, hii ilifunga milango ya ushirikiano.
Barua nyingine, kutoka uongozi wa FBME sehemu ya Ukaguzi wa Ndani, ‘Risk’ na ‘Compliance’ na idara ya usalama wa Taarifa iliyotumwa tarehe 16 Machi, ilikwenda moja kwa moja CBC na kudai kwamba walikuwa wakizuiwa kutekeleza wajibu wao na kutohusishwa katika maamuzi ya mpango mkakati. Kwa hili, majibu yalikuwa tofauti. Waliitwa kwenye ofisi ya msimamizi na kutishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu hawakupitia kwa msimamizi mwenyewe. Hakuna chochote kilichofanyika kwa wakati ule ama baadae kuhusiana na maombi yao – ambayo hayajatekelezwa – au hatari iliyowakabili kwa kutotekeleza majukumu muhimu waliyokabidhiwa.
Kama angefikiria kushirikiana na uongozi wa FBME badala ya kuwa kinyume chake daima!
Mameneja wengi wa FBME Cyprus na wamiliki wapo kwenye jengo moja na msimamizi mpya, wakati viongozi waandamizi wa Benki Kuu wapo mita mia kadhaa tu kwenye jingo zuri la CBC.
Hakika, sio mbali kuzidi upeo wa binadamu na kuamua kukaa na kuongea!