Ufafanuzi: Maamuzi ya Mwisho Yaliyo Mbali na Mwisho

Machi 27, 2016

Maamuzi yanayosemekana kwamba ni ya “Mwisho” yaliyochapishwa na FinCEN Ijumaa, Machi 25, 2016, sio kweli kabisa kwamba ni ya “mwisho”. Bado yapo chini ya amri ya zuio la awali la mahakama ya shirikisho ya Washington DC ambayo inazuia maamuzi haya kufanya kazi na kuleta athari ikisubiri uchunguzi zaidi wa mahakama hiyo katika masuala ya haki, usahihi na uhalali wa mchakato wa FinCEN. “Maamuzi ya Mwisho” pia yana masharti yake yenyewe, kwamba ni lazima yasubiri kipindi cha miezi mine baada ya kuchapishwa rasmi na tarehe ya utekelezaji wa maamuzi hayo. FBME ina haki zote na nia ya kupinga uhalali wa “Maamuzi ya Mwisho” ili mahakama ya Marekani iweze kuamua kama ni halali maamuzi hayo kufanya kazi.

Wala madai ya FinCEN kwenye “Maamuzi ya Mwisho” hayajabadili jambo lolote ukilinganisha na madai ya awali yaliyosababisha zuio la mahakama. FinCEN wamerudia makosa yaleyale na kuleta tena ushahidi wa kiujanja ujanja kwenye maamuzi yake ya Mwisho. Makosa haya – yanayoleta masikitiko lakini yaliyotarajiwa yanaipeleka FinCEN kwenye maamuzi potofu ya sheria maalum inayoitwa “Fifth Measure”. Tunadhani ni dhahiri kwamba kwa hatua hii FinCEN imeonyesha ukaidi mkubwa kwenye hitimisho lake lisilofuata taratibu za ushahidi, ukweli, sheria, maoni ya umma, au kusimama kwenye misingi ya usawa.

Pongezi kwa mfumo wa kimahakama, ratiba, na zuio la muda lililopo, hata hivyo, siku ya mahakama ya FBME inakaribia. Tunasisitiza kwamba tuna kila nia ya kuipinga FinCEN kwenye Maamuzi yake ya Mwisho kwani yana kasoro kubwa kimchakato na yasiyo na mantiki na tunaisubiri kwa hamu siku ya mahakama.