Februari 27, 2015
Kwa niaba ya wote wanaohusiana na Benki ya FBME, tovuti hii inaishukuru Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na Msimamizi wake kwa kusimamisha tozo ya adhabu kwa FBME kwa kuwa na kiwango cha juu cha fedha kuliko kinachotakiwa na CBC. Mbali na kusitisha tozo hiyo, CBC pia imerudisha fedha ya adhabu iliyoichukua katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Wamefanya kazi nzuri.
Kuna takriban EUR 160,000,000 – fedha za Benki ya FBME zinazoshikiliwa na CBC (kwa takwimu za sasa). Benki kuu alichukua hatua ya pekee kupata fedha hizo kutoka fedha za ukwasi za FBME bila kuishauri FBME wala Benki Kuu ya Tanzania, ambapo ni makao ya Msimamizi Mkuu.
Tamko la kwanza kutoka mahakama ya usuluhishi ilikuwa kuacha kutumia fedha za FBME zilizoko CBC.
Utaratibu wa kawaida ni kwamba mabenki yote yanatakiwa kuwa na 1% ya fedha za amana yake. Katika uamuzi wa Benki Kuu ya Ulaya ambayo CBC ni mwanachama, kuna adhabu kwa fedha yote inayozidi kiwango hicho kilichopo kwenye Benki Kuu. Hii ni kuhakikisha kwamba benki zinatumia fedha zao katika jamii kusaidia upunguzaji wa makali ya kiuchumi yaliyoikumba jumuiya hiyo. Kiwango cha adhabu ni 0.2%. Adhabu hii haikutakiwa kamwe kulipwa kwa sababu FBME haikuwa na usemi katika suala hilo. Kwa sasa, kasoro hii imetambuliwa na CBC na adhabu kuondolewa.
Kama inavyoonekana kwingine, Mahakama ya Usuluhishi ICC imetoa wito kwa CBC kusimamisha baadhi ya hatua zilizodhamiria kuzichukua dhidi ya tawi la FBME la Cyprus. Hatua nyingine ambayo Mahakama imeweka msisitizo ni kutochukua hatua zaidi kwenye hoja ya kuuza tawi la Benki ya FBME la Cyprus.
Haijaelezwa kamwe na CBC uhalali wa kuuza au hata kutoa upembuzi yakinifu.
Katika kipindi tangu CBC kutangaza nia yake Julai iliyopita, hakuna muuzaji au mnunuzi aliyejitokeza licha ya madai ya mara kwa mara yaliyodai hivyo. Sasa, chanzo kisichofahamika kutoka CBC kimenukuliwa na gazeti la Cyprus Mail, Februari 25 ukurasa wa 5, kikisema kuwa jaribio la kupata mnunuzi “… limeonekana gumu kwa sababu uwepo wa FBME Cyprus ni tawi tu na inakosa mali halisia mbali na majengo, samani na vifaa vingine “.