Mahakama ya Cyprus Yaizuia CBC Kubatilisha Leseni

Januari 19, 2016

Mahakama nchini Cyprus imeamuru kusimamisha hatua iliyochukuliwa na Mdhibiti wa benki yenye lengo la kuifilisi Benki ya FBME tawi la Cyprus. Hii inafuatia jaribio la kufutiwa leseni ya tawi lililotangwa kwa umma na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) tarehe 21 Desemba 2015.

Usitishwaji huu wa leseni na baadae jaribiola la hatua za kisheria (ex parte) lililofanywa na CBC yamepingwa vikali na FBME, ambayo imeanzisha mapambano ya kisheria chini Cyprus kwenye  ‘Mahakama Kuu na Mahakama ya Wilaya ya Nicosia.

Lau kama hatua hizo za kisheria zingetumika kufanya hukumu ya kesi na kufanikiwa, ingemaanisha kwamba tawi la FBME lingefilisiwa bila  kushauriwa au kupewa nafasi ya kupinga hoja hiyo. Kwa furaha ya mchakato wa kimahakama, Mahakama Kuu imekataa hoja hiyo, na hivyo kusababisha mlolongo wa taratibu za kisheria kati ya CBC na leseni ya FBME ambayo inaanza tarehe 19 Januari.

Kupitia tovuti hii, FBME itawapasha habari juu ya maendeleo ya sakata hili wale wote wanaofuatilia.