Novemba 6, 2015
Vyanzo vya habari vinavyopinga hatua zilizochukuliwa na kundi dogo la maafisa wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC) dhidi ya Benki ya FBME, vimetahadharisha kwamba CBC inapanga kufilisi tawi la FBME la Cyprus kufuatia taarifa ya FBME kuhusu uamuzi wake wa kuhamisha baadhi ya akaunti za wateja wake kutoka tawi lake la Cyprus kwenda makao Makuu – Tanzania. Lengo likiwa kujinasua kwenye mtego wao wenyewe. Kama ikitekelezwa, hatua hii ya hatari na haramu itapingwa vikali kwa kutumia vifungu mahsusi vya kisheria.
Kufilisi kunahitaji tawi kukosa ukwasi, kitu ambacho hakipo kwa kesi inayohusiana na FBME ambayo ina ukwasi wa kutosha kama inavyofahamika na wote, ikiwa ni pamoja na CBC.
Benki ya FBME pia inapenda kurudia uamuzi wake wa kuhakikisha kwamba amana zote zilizopo katika tawi la Cyprus zitalindwa dhidi ya udhalimu wa CBC. Hila hii ya CBC inakuja wakati ambapo FBME imependekeza kuhamisha akaunti za wateja ‘watakaopenda’ kutoka tawi la Cyprus kwenda makao Makuu ya Benki yaliyopo Tanzania kama njia ya kuwapa wateja uwezo wa kupata fedha zao.
Barua iliyotumwa kwa Benki ya FBME tarehe 30 Oktoba na kusainiwa na Gavana wa CBC, Chrystalla Georghadji, inaiagiza Benki Kuu ya Tanzania na Benki ya FBME kuwasiliana na mabenki waambata wao ili kupeleka fedha zote CBC. BOT and FBME Makao Makuu wanapinga uamuzi huu kutokana na tuhuma ya nia ya CBC kutokana na jinsi ilivyoshughulikia masuala ya Benki ya FBME kwa kipindi cha miezi 15.
Barua hiyo inadai kuwa inaegemea kwenye kumbukumbu ya makubaliano yaliyofikiwa Agosti 11, 2015 kati ya CBC na Benki Kuu ya Tanzania, nakala ambayo FBME imeiomba kutoka CBC lakini haijapatikana hadi sasa. Aidha, barua kutoka CBC inatoa tarehe ya mwisho kuwa November 5, kitu kinachotoa ushahidi wa ziada wa mpango dhalimu wa CBC, ambao unatengenezwa ili kufunika kitendo haramu na kisicho cha kisheria cha kufilisi.
Afisa wa CBC anayehusika na hila hii ni mtu anayeripoti kwa Gavana na Mkurugenzi Mwandamizi wa CBC, wote wawili wakiwa hawana uzoefu na Benki. Aidha, wajumbe waliobakia wa bodi ya CBC (wamebakia wanne kati ya nane walioteuliwa awali) ambao pia ni wajumbe wa Mamlaka ya Usuluhishi. Hawa wote wanaongozwa na ushauri kutoka kwa Michalis Stylianou, ambaye anaongoza Kitengo cha mtu mmoja cha Usuluhishi na ambaye anatakiwa kujua anachokifanya.