Novemba 8, 2015
Pongezi kwa mfumo wa kimahakama wa Marekani, FinCEN imesitishwa kutekeleza maamuzi yake ya kuiwekea vikwazo Benki ya FBME vilivyotishia kuibomoa kabisa ingawaje FBME imekuwa ikishughulikia masuala yote yaliyoibuliwa na mamlaka husika au wakaguzi. Bila maamuzi ya Jaji Cooper, FinCEN ingeweza kuifuta Benki kabisa kutokana na ushahidi ambao FinCEN walisisitiza kuwa ni siri, licha ya ukweli kwamba hakukuwa na msingi halali kisheria wa kuuzuia ushahidi huo.
Benki ya FBME inahitaji tu nafasi ya kukabiliana na angalau baadhi ya ushahidi huo wa siri ili kusafisha jina lake, na kulinda wafanyakazi wake na wateja.
Inafurahisha kuona kwamba Jaji Cooper, kwa kutoa hukumu hii ya Novemba 6, ametoa miezi minne kwa FinCEN kukamilisha upya mchakato,wake wa kimaamuzi huku ikizingatia mipaka ya sheria na wakati huo huo amri ya zuio ya mahakama yake ikiendelea.. Jambo jingine muhimu, Jaji Cooper imekubali kwamba FinCEN ina wajibu “chini ya sheria ya Utaratibu, kutoa taarifa zisizolindwa na Sheria ya Usiri wa Kibenki inapotarajia kuegemea”.
FBME inadhani kwamba FinCEN wangetambua wajibu huu katika hatua za awali. Na FBME anasubiri kwa hamu kutoa maoni yake kwenye taarifa za siri zilizokuwa zinashikiliwa na FinCEN huku ikitambua, kama Jaji Cooper alivyosema, kwamba FinCEN sasa itaangalia upya maeneo yote na vielelezo kuhusu hukumu ya FBME.