Gavana wa zamani wa CBC Ashangazwa na Maamuzi ya FinCEN

Februari 11, 2016

Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC), Profesa Panicos Demetriades, amewaandikia FinCEN kuhusu kampeni yake dhidi ya FBME ambapo anasema “… anashangazwa sana na vitendo vya FinCEN kwa FBME”. Barua hii inaonekana kwenye tovuti ya FinCEN na inapatikana kwa umma kwenye anuani: http://www.regulations.gov/#!documentDetail;D=FINCEN-2014-0007-0069.

Profesa Demetriades alikuwa Gavana wa CBC kuanzia Mei 2012 hadi Aprili 2014, kipindi kifupi kabla ya kuchapishwa kwa madai ya FinCEN dhidi ya FBME (Julai 2014). Katika barua yake anauliza ni ushahidi gani wa maana uliopo dhidi ya FBME na kuamini kwamba FBME inaweza kufanywa “kafara” kwa “siasa potofu” za Cyprus.

“Wakati nilipokuwa Gavana wa CBC … Mfumo wa CBC wa Upambanaji na Fedha Chafu (AML) uliboreshwa na kuwa imara sana,” aliandika. “Pamoja na uboreshaji wa sheria za AML, hakuna wakati ambapo nililetewa ushahidi wowote unaoonyesha kwamba benki flani ya Cyprus imeshiriki katika kutakatisha fedha chafu katika kipindi hicho.

“Kwa yaliyoandikwa hapo juu, nimeshangazwa sana na vitendo vya FinCEN dhidi ya FBME. Nilishangaa kusikia FBME inatangazwa na FinCEN kuwa ni chombo cha ‘msingi cha kusafishia fedha chafu’. Je, kuna ushahidi madhubuti unaounga mkono madai makubwa kama haya? Au yanatokana na uvumi na tetesi, kutoka kwa washindani wa benki hiyo nchini Cyprus na / au wasaidizi wao wa kisiasa?

Katika barua yake Panicos Demetriades anaelezea kuwa matukio mengi nchini Cyprus ni mwendelezo wa siasa za vyama yanayoendeshwa na makundi maalum ya kimaslahi. “Wakati wa uongozi wangu, kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba baadhi ya wanasiasa walikuwa wanakerwa na uwepo wa FBME nchini Cyprus.

“Benki ndogo kama FBME, pamoja na kuwa chanzo cha ushindani bora, lakini bila kukusudia ni tishio kwa mendeleo ya mabenki makubwa. Kwa hiyo, huwa yanavutia ushawishi wa wanasiasa, mara nyingi kwa sababu za uongo. Kabla ya uteuzi wangu, Benki ya FBME, iliamua kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwa kununua hati fungani za Cyprus, uwekezaji ambao ulisaidia nchi ya Cyprus kuepuka kufilisiwa wakati wa mazungumzo na kundi la Uropa (Eurogroup) na IMF katika nusu ya pili ya 2012 na mwanzoni mwa 2013.

“Si jambo lisilokubalika; na hakika kuna uwezekano, kwamba wanasiasa waliokuwa katika upinzani wakati huo walitafsiri hatua hii kama kuikomboa serikali iliyopita. Hivyo, pamoja na FBME kuendelea kuifadhili nchi hata baada ya mabadiliko ya utawala, baadhi ya wanasiasa wa chama tawala wanaweza kuendelea kuiona FBME kama benki hasidi, “aliongeza Profesa Demetriades.

“Pia nina wasiwasi kwamba FinCEN yenyewe inawezekana imepokea taarifa za kupotosha au zisizo sahihi kuhusu FBME kutoka vyanzo vya Cyprus, kwani benki ndogo kama FBME inaweza kufanywa kafara kirahisi.”

Profesa Panicos Demetriades sasa ni Profesa wa Uchumi wa Fedha katika Chuo Kikuu cha Leicester nchini Uingereza.