Januari 26, 2015
Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara mjini Paris imekubaliana juu ya uteuzi wa jopo la wasuluhishi walioteuliwa na wamiliki wa Benki ya FBME, Jamhuri ya Cyprus na mwenyekiti wa mahakama. Moja ya kazi ya kwanza kwa wasuluhishi hao ni kuangalia kwa haraka suala la madhara yaliyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus kufuatia kukubaliwa kwa shauri la usuluhishi na ICC tarehe 28 Oktoba 2014.
Jopo la watu watatu wa mahakama linaundwa na Profesa Pierre Tercier (mwenyekiti), Profesa Ibrahim Fadlallah na VV Veeder QC.
Profesa Pierre Tercier anaheshimiwa sana kama mwenyekiti wa zamani wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Chama cha Kimataifa cha Biashara. Yeye ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Fribourg na Profesa anayetembelea vyuo vikuu vingine mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Geneva na Paris. Ana uzoefu mkubwa wa usuluhishi wa kimataifa na utatuzi wa migogoro.
Profesa Ibrahim Fadlallah ni Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Paris. Amefanya kazi kama msuluhishi au mshauri katika kesi mbalimbali za usuluhishi mara kwa mara na chini ya Kanuni za ICC, ICSID, Chama cha Usuluhishi cha Ufaransa, na Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya. Ni mwanachama wa zamani wa mahakama ya ICC na mwanachama wa Baraza la Taasisi ya Sheria ya Biashara ya Dunia. Pia ni mwanachama mwanzilishi wa Usuluhishi kati ya mataifa ya Kiarabu na Ulaya na mwanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya sheria. Mr VV Veeder QC anafanya kazi kama msuluhishi na mshauri wa kisheria kutoka Mahakama ya Essex Chambers London. Yeye ni mwanachama wa Bodi ya Uongozi ya ICCA na Taasisi ya Usuluhishi ya Chama cha Wafanyabiashara Stockholm. Ni mtaalamu katika sheria za biashara na biashara ya nje ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa kimataifa, benki na sheria za fedha.
Chemba ya Kimataifa ya Biashara (ICC) ni shirika kubwa linalowakilisha masuala ya biashara duniani. ICC ina shughuli kuu tatu: kuweka misingi ya utawala, utatuzi wa migogoro, na uenezaji wa sera. Kwa sababu wanachama wake ni makampuni na vyama vinavyojihusisha katika biashara ya kimataifa, ICC ina mamlaka makubwa katika uundaji wa sheria zinazotawala na kusimamia uendeshaji wa biashara na mikataba kwenye nchi mbalimbali.