Mafunzo ya Kuzuia Utakatisishaji wa Fedha haramu na Kufadhili Ugaidi (AML na CTF)

Januari 23, 2015

Kama sehemu ya ahadi yake kwa FinCEN, Benki ya FBME itafanya upya mafunzo kwa wafanyakazi ili kuonyesha ahadi yake ya utekelezaji wa udhibiti wa mifumo ya benki wakati wote. Mafunzo haya mapya yataongeza elimu ambayo tayari wafanyakazi wanayo na itazidisha mifumo ya udhibiti wa Benki. Lengo hasa ni sera ya kukabiliana na kupambana na fedha haramu, jua-mteja-wako, kukabiliana na kufadhili ugaidi na vikwazo vya kiuchumi.

Mafunzo haya yatatokana na kitabu cha ushauri chenye kurasa 46. Kutakuwa na mtihani kwa wafanyakazi wa Benki ya FBME, ambayo inaleta njia bunifu za kuchukua katika hali tofauti. Kozi hii itabainisha masuala yanavyoshirikishwa na inaonyesha jinsi ya kutambua ukiukaji wa kanuni. Kutakuwa na maelezo ya jukumu la Benki na itaainisha majukumu yanayowahusu wafanyakazi wote.

EY (Ernst and Young) ilisha dhihirisha kuwa benki ya FBME ilikuwa na udhibiti wakati ilipofanya uchunguzi wa kihasibu hapo Benki. Katika tathmini yake, EY ilisema: “Sera na taratibu za kupambana na pesa haramu (AML) za FBME ziko sambamba na maelekezo husika (ya EU na Benki Kuu ya Cyprus)”. Hata hivyo, EY na wawakilishi wa Benki wa kisheria, Hogan Lovells, walitoa mapendekezo ya kuimarisha mipango, ambayo Benki imeipitisha kikamilifu. Mafunzo haya ya marejeo yanadhihirisha hili.

FBME kwa wakati wote, inasema, Benki ina nia ya kufanya biashara yake kwa mujibu wa sheria na kanuni zote husika. Kufuata kanuni ni wajibu wa kila mtu katika FBME na mafunzo haya rejea ni sehemu ya njia ambayo kila mfanyakazi atashiriki katika ahadi hii.

———————-

Mfumo wa kisheria na udhibiti wa Cyprus una sheria na kanuni zifuatazo za AML / CTF:

  • Kuzuia na Kupambana na Shughuli za Fedha haramu, Sheria ya 2007-2013
  • Maelekezo ya Benki Kuu ya Cyprus kwa Taasisi ya Mikopo, toleo la (Desemba 2013)
  • Kanuni 1781/2006 la Bunge la Ulaya na baraza la Novemba 15, 2006 juu ya Taarifa juu ya Mlipaji na uhamishaji wa Fedha