Desemba 28, 2015
Mwenyekiti wa Benki ya FBME, Bwana Ayoub-Farid M Saab, ameandika Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Cyprus, Nicos Anatasiades, kuonyesha madhara makubwa yaliyosababishwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC). Vitendo vya karibuni vya CBC ni pamoja na jaribio la kuifutia leseni, si tu kwa tawi la FBME Cyprus, bali kwa Tanzania pia.
Inatoa wito kuwa uchunguzi wa maafisa wa CBC, ulioanzishwa majira ya machipuko ya 2015 na ‘Baraza la Wawakilishi’ la Cyprus uendelezwe haraka ili kuepuka kundi dogo la maofisa kutoleta madhara zaidi kwa nchi, CBC au kwa FBME. Barua inasema kwamba maamuzi ya hivi karibuni ya CBC yamesababishwa na kushindwa kwa kesi yake katika mahakama ya kimataifa nchini Marekani na Ufaransa, na kukatishwa tamaa kwa ‘matokeo mabaya kwao’. Barua inaeleza nia ya FBME kushiriki katika majadiliano ya kutafuta suluhisho la tatizo lililopo.
Nakala kamili ya barua inapatikana hapa