Ukwasi Waongezeka

Novemba 20, 2014

Zaidi ya taarifa yetu asubuhi hii, ni vizuri kuwaeleza kwamba kiasi kikubwa kutoka akaunti ya FBME Bank kimewasili katika Benki Kuu ya Cyprus. Hivyo, kwa sasa, suala la ukwasi halipo tena na miamala inatakiwa ianze. Ni vizuri kuleta habari za ukaribisho kwa wateja wetu, wafanyakazi, benki waambata, na marafiki. Tunatumaini kwamba Benki Kuu ya Cyprus itazingatia akilini mwao wakati wakichukua ushuru kwa FBME Benki. Kwa sheria ya ECB, fedha zinazotakiwa kubaki kwenye mamlaka ya udhibiti isizidi 1% ya amana ya jumla ya benki. Kwa uangalifu mkubwa, ECB inataka fedha za benki zitolewe katika ukanda wa euro zifanye kazi na watu na makampuni kusaidia kujenga upya uchumi uliodorora. Fedha itayowekwa katika benki kuu na taasisi binafsi zaidi ya 1% itatozwa faini kwa kiwango cha sasa cha 0.2%.

Kiukweli, kwa hali hii ambapo fedha za tawi la FBME zilizopo kwenye Benki Kuu ya Cyprus chini ya maagizo ya msimamizi wake mwenyewe hazipaswi kuwa chini ya sheria hii, kwa sababu FBME haina usemi juu ya suala hili. Hata hivyo miezi ya Agosti, Septemba na Oktoba faini hiyo ilitozwa. Pongezi kwa msimamizi, Dinos Christofides, ambae amesema atalifanyia kazi suala hili ili fedha hizo zirudishwe. Tunatarajia hili litafanyika kabla ya muda mrefu.