Hatua Zinaendelea Kupata Ukwasi wa Ziada

Novemba 20, 2014

Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Meneja Msimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania na Benki ya FBME Dar Es Salaam, FBME Limited inachukua hatua za kupata ukwasi wa ziada kwenye tawi la FBME Cyprus. Hii inafanywa ili kuhakikisha uwepo wa amana ya kutosha kwa wateja kuepuka tatizo la kiwango cha siku cha muamala kilichowekwa na msimamizi aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus.


Viwango hivi vilianza kwa EUR 10,000 kwa siku, kisha EUR 5,000 na kwa sasa kimepunguzwa hadi EUR 2,000. Viwango hivi viliwekwa kufanya kazi gani hasa? Mbali na matumizi ya nguvu kwa ajili yao mwenyewe, haijaweza kuwasaidia wateja, tofauti ya yanayosemwa.

Kama inavyoeleweka, ukwasi wa kutosha upo katika Benki ya FBME kwa ujumla. Benki imebakia kuwa tunda bora kama ilivyokuwa Julai. Juhudi zinazofanywa na FBME Ltd na Benki Kuu ya Tanzania zitaweka huru fedha kwa ajili ya wateja wa tawi la Cyprus, ikiwa watapata ushirikiano wa msimamizi na wakubwa zake katika Benki Kuu ya Cyprus. Hata hivyo, kwa wakati huu hili halina dalili ya kutokea.

Hatimaye, mtu atafikiria kwamba jukumu la msingi la Benki Kuu ni kulinda mfumo wa benki na wateja wake, hivyo ni vipi ukosefu wa sasa wa ushirikiano unaweza kusaidia kufikia lengo hili? Tunahofia mageni zaidi kutoka mtaa wa Kenedy.