Vyombo vya Habari Vyabaini Sababu za Ukiritimba Kwenye Soko la Kadi

Juni 22, 2015

Taarifa kutoka magazeti ya Cyprus yamebaini uhusiano kati ya kupanda kwa bei katika soko la walaji na kuanza kwa mazoea ya ukiritimba kwa Kampuni ya Malipo ya JCC . Taarifa hizi zimepatikana katika gazeti la Politis toleo la 17 Juni na Simerini toleo la 18 Juni.

 

JCC imekuwa kampuni pekee inayofanya biashara ya kupokea manunuzi yanayofanywa kwa kadi nchini tangu kitengo cha huduma ya Kadi cha FBME kilipolazimika kuahirisha shughuli zake Agosti mwaka jana. Kampuni ilichukua uamuzi huu, na kuwapunguza kazi robo tatu ya wafanyakazi wake, yakiwa ni matokeo ya moja kwa moja ya hatua ya Azimio iliyowekewa tawi la FBME la Cyprus. Wakishindwa kupata huduma ya akaunti ya benki ya FBME kutokana na kufungwa kwa tawi na Benki Kuu ya Cyprus, na kisha kufunguliwa kwa muda, Kitengo cha Kadi cha FBME hakikuweza kuendelea.

 Hii iliiacha JCC kuwa shirika pekee katika Jamhuri lenye uwezo wa kufanya malipo kwa kadi. Kwa mujibu wa Politis, ada za JCC zimepanda. “Utafiti wa wafanyabiashara umeonyesha ada zimepanda kwa kiasi cha 0.25% – na kusababisha kupanda kwa bei za watumiaji,” taarifa hiyo ilisema ikiongeza kuwa gharama za matumizi ya kadi nchini Cyprus kwa sasa zipo juu ukilinganisha na nchi za ukanda wa Ulaya. Aidha, inaaminika JCC inatumia vitisho vya adhabu kubwa kuwalazimisha wafanyabiashara kusaini mikataba ya muda mrefu kama njia ya kuendeleza ukiritimba wake.

 JCC, ambayo inamilikiwa na muungano wa mabenki, ilianzishwa mwaka 1989 na kufurahia ukiritimba hadi kuwasili kwa Kitengo cha Huduma za Kadi cha FBME mwaka 2009. Kuwepo kwa ushindani katika soko mara moja kulianza kushinikiza bei kushuka. Inasemekana JCC ilianza kujibu kwa vitendo vya kupambana na ushindani ambavyo vililalamikiwa kwenye Tume ya Jamhuri ya Ulinzi wa Ushindani. Uchunguzi ulianzishwa na mnamo Aprili 2014 Tume ilitoa uamuzi wake wa awali na kugundua kwamba JCC ilikuwa “ikizuia ushindani” na tabia yake hiyo “ilivunja sheria kwenye ibara ya 3 na 101 ya Mkataba wa Utendaji kazi wa Umoja wa Ulaya”.

 Kesi hiyo iliendelea Februari na Machi mwaka huu, na Tume inatarajiwa kutangaza uamuzi wake wa mwisho kuhusu mwenendo wa JCC kabla ya majira ya joto hayajaisha.

 Mbali na madhara ya bei wanayopata walaji wanapofanya malipo ya kielektroniki, magazeti yote mawili yalionyesha uhusiano kati ya kesi hii na hatua ya Azimio zilizowekwa na Benki Kuu ya Cyprus kwa FBME tawi la Cyprus.

 Kwa viunganishi kwa lugha ya Kigiriki katika gazeti la Simerini bofya hapa, kwa lugha ya Kiingereza kwenye gazeti la Cyprus Weekly Bofya hapa