Wafanyakazi Hawahusiki

3 May 2015

Taarifa za hivi karibuni zilieleza kimakosa kuwa wafanyakazi wa FBME wamekwenda Polisi na Benki Kuu ya Cyprus kupeleka madai yasioeleweka kuhusiana na ukiukwaji wa mfumo wa kupambana na pesa chafu. Ukweli ambao FBME inauelewa ni kwamba, watu wanaozungumziwa ni watu binafsi wanaohusishwa na makampuni ya Uingereza ambayo kwa sasa wako katika madai na FBME kuhusu mgogoro wa ankara zilizokataliwa na huduma.

Watu hao walikuwa wakitoa huduma za uchunguzi kwa wanasheria wa nje ili kuwasaidia katika kesi za kisheria. Walisitishiwa kazi hiyo kwa madai ya ubora na uadilifu wa kazi zao, ukubwa wa ankara zao na wasiwasi fulani juu ya shughuli zao za siku za nyuma na ushiriki wao kwenye biashara ambavyo hatimaye FBME imevibaini. Upataji wao wa taarifa ulikuwa ukifuatiliwa kwa makini na kudhibitiwa na iwapo wanataka kutumia vibaya taarifa za siri tunawathibitishia kwamba juhudi hizo hazitaathiri wateja wetu. Tunatambua pia kuwa nyaraka hizi ni za zamani, na kama watu hao (wawili) wenyewe wanavyosema, nyaraka hizi hazihusiani na hali ya sasa ya kadhia ya AML ilioyopo FBME.

Tunafahamu kwamba watu hao wameiajiri kampuni ya sheria ya Cyprus ambayo pia inaiwakilisha kampuni ambayo Kitengo cha Huduma za Kadi cha FBME kimeshitakiana nayo na wameiomba Benki Kuu ya Cyprus katika kujaribu kuiruhusu ifanye nayo kazi.

FBME imeitahadharisha Benki Kuu kuhusu watu hawa lakini, inaonekana, maslahi pekee ya Benki Kuu ni kufungwa kwa FBME kwa gharama yoyote ili kuhalalisha vitendo viovu vya Benki Kuu yenyewe.

Kueleza ukweli, tunaona kwamba baada ya miezi tisa ambapo CBC imeidhibiti kikamilifu Benki ya FBME tawi la Cyprus lenye msimamizi anaelipwa (€ 10,000), na licha ya kaguzi nyingi ambazo CBC imezifanya, sasa imeamua kuteua Msimamizi Maalum mwingine anaelipwa ada ya kila mwezi (50,000 € pamoja na nyongeza ya 20% kwa ajili ya matumizi mengine – ndiyo, kiasi ni sahihi!) na kufanya ukaguzi mmoja zaidi wa mfumo wa AML wa FBME. CBC haijawahi kuweka matokeo ya kaguzi zake zote zilizopita kwa FinCEN kusaidia katika kusafisha jina la FBME. Wala haijaeleza ni kwa nini ikiwa hii ni mara ya kwanza katika miaka 32 ya usimamizi iliona ni muhimu kuwashirikisha polisi.

Mlolongo huu wa shughuli kwa umma inaonekana kuwa ni jaribio la kukwepesha mtazamo wa umma kwa uzembe wa Benki Kuu ya Cyprus uliodumu kwa miezi tisa mfululizo kuhalalisha kutokuchukua hatua kwa muda mrefu na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya usimamizi.

Tutaendelea kutoa taarifa mpya juu ya jambo hili ambapo wasomaji wataweza kutoa maamuzi wao wenyewe.