Wasimamizi Wawili wa FBME Kulipwa zaidi ya Gavana wa CBC na Mario Draghi – Kwa Pamoja

Mei 5, 2015

Ukweli wa mambo umeibuka kutokana na maelezo ya uteuzi wa msimamizi wa pili wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kuendesha tawi la Benki ya FBME la Cyprus. Wasimamizi hawa wawili wanalipwa zaidi ya mishahara (kwa pamoja) ya Gavana wa CBC na mtu anayemtambua kama bosi wake, Rais wa Benki Kuu ya Ulaya – ECB, Mario Draghi. Pengine unaweza pia kuunganisha mishahara ya wafanyakazi wengine wa Bodi ya Wakurugenzi ya CBC na bado ukabaki na chenji.

Msimamizi wa kwanza, Dinos Christofides, anachukua hundi ya EUR 10,000 kila mwezi (EUR 120,000 kwa mwaka), wakati wa pili, Andrew Andronikou analipwa EUR 50,000 kwa mwezi (EUR 600,000 kwa mwaka) na ziada ya 20% kwa ajili ya gharama walizokubaliana. Malipo yote yanakatwa kutoka amana za FBME zilizopo CBC na wamiliki na wakurugenzi wa FBME hawana la kusema katika maamuzi hayo.

Msimamizi wa pili, Andrew Andronikou amechukua nafasi yake Alhamisi iliyopita, 30 Aprili, baada ya miezi tisa ya kutokuchukua hatua na mara nyingine uongozi wa kisasi na uzembe toka kwa msimamizi wa kwanza, Dinos Christofides. Ameteuliwa kufanya kazi “kiushirika” na Christofides. Katika mkutano wake na wafanyakazi siku ya Alhamisi 30 Aprili, Andronikou alisema “hakuna kilichobadilika,” na “Jumatatu ni biashara kama kawaida -! Hadi kitu kitakapotokea”

Hiyo ina maana kiwango cha malipo kwa wateja kinabakia kilekile EUR 200 kwa siku ya kazi, ambacho kwa upande mwingine kimesababisha malipo ya mishahara ya mashirika kwa wafanyakazi wao kutolipwa kwa wakati.

Kwa mujibu wa Idara ya Huduma ya Takwimu ya Wizara ya Fedha mapato ya wastani ya kila mwezi kwa Wacyprioti kwenye robo ya nne (Q4) ya 2014 (hubadilika kila robo mwaka) ilikuwa EUR 1862. Dinos Christofides analipwa mara tano zaidi ya wastani wa mshahara kila mwezi wa Mcyprioti. (Labda pungufu kidogo kama amefanikiwa kurekebisha kiwango cha kodi yake baada ya miezi tisa), wakati Andrew Andronikou analipwa mara 26 zaidi ya wastani wa Mcyprioti anazolipwa kwenye hundi yake ya kila mwezi.

Baada ya mazungumzo yaliyotangazwa sana, Chrystalla Georghadji, Gavana wa Benki Kuu ya Cyprus, hatimaye alifanikiwa mshahara wa EUR 9,500 kila mwezi (EUR 114,000 kwa mwaka kama ilivyokubaliwa Novemba 29, 2014).

Bosi wake, Mario Draghi, Gavana wa Benki Kuu ya Ulaya analipwa mshahara wa EUR 31,634 kwa mwezi (EUR 379,608 kwa mwaka kama ilivyoripotiwa kwenye ripoti ya mwaka ya ECB 2014).

Benki ya FBME haikukubaliana na wasimamizi hawa lakini inalazimishwa kuwalipa kiasi kikubwa kuliko mishahara ya Rais wa ECB, Gavana wa CBC na Wakurugenzi wengi wa Bodi kwa pamoja. Chrystalla Georghadji ni lazima aamini kwamba wasimamizi hawa ni muhimu sana hadi kuhalalisha malipo yao.