Mamlaka ya Azimio Yaelea Kwenye Bahari ya Matatizo

Machi 12, 2015

   Tafakari juu ya kazi ya Mamlaka ya na Kamati ya Azimio ya Cyprus.

Mamlaka ya Azimio na Kamati ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) wanaandamwa na vyombo vya habari kwa wakati huu, na hakuna hata chombo kimoja kilicho kwenye upande wake. Linalozungumzswa sasa ni kuhusu Utawala wa benki iliyofungwa ya Laiki, ambapo wamiliki wake wa akaunti wa Cyprus wamepata hasara kubwa ya mamia ya mamilioni ya Euro. Linaloleta mgogoro kwa sasa ni kuhusu hatua ya kisheria ya Mamlaka ya Azimio dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Benki ya Laiki, Andreas Vgenopoulos. Msimamizi iliyeteuliwa kushughulikia Azimio la Laiki, Andri Antoniades, alijiuzulu Jumatatu Machi 2, na kuwalaumu Gavana wa Benki Kuu na Mamlaka ya Azimio kwa masuala ya kijinga yanayohusishwa na kesi za kisheria, ikiwa ni pamoja madai kwamba binti wa Gavana bado analipwa mshahara na Mwenyekiti wa zamani wa Laiki pamoja na ahadi zilizotolewa mapema kuwa angejiuzulu. 

Mamlaka ya Azimio na Kamati yake zimeaibika. Ni ubovu wa kiasi gani utakaoruhusiwa kuendelea na kuwaumiza walipakodo maskini wa Cyprus, wadeni wa Laiki na wateja wa FBME wa tawi la Cyprus, bado ni kitendawili.

Tunadhani ni wakati muafaka kuwaeleza wasomaji jinsi Mamlaka ya Azimio na Kitengo chake cha Kamati ya Azimio.

Mamlaka ya Azimio ilianzishwa mwaka 2013 wakati Benki ya Laiki ilipokufa na kufanya Sekta yote ya Benki ya Cyprus kutikisika. Mamlaka inaundwa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa CBC.

Hadi leo hii, Kamati ya Azimio ilijumuisha wajumbe watatu wa bodi ya CBC; Gavana, Chrystalla Georghadji (Mkaguzi Mkuu wa zamani), na Wakurugenzi wake watendaji wawili, George Syrichas na Stelios Kiliaris (wachumi na wasomi). Kwa sasa, Mr Kiliaris ameripotiwa kujiuzulu, akitoa sababu za rushwa, ghasia na uzembe ndani ya Benki Kuu. Kati ya wajumbe hawa watatu, hakuna ambae amekwishafanya kazi benki.

Hakuna hata mjumbe mmoja kutoka nje ya CBC. Hii ni kile kinachoitwa ‘Mkono mmoja Kuuosha mwingine’ na imesababisha utawala mbovu kwenye kila jambo linalotokea. Kinadharia, Waziri wa Fedha anaweza kutumia veto juu ya maamuzi makubwa yanayopendekezwa na Mamlaka ya Azimio, lakini, kama tulivyoona, mamlaka hii haina meno ukichukulia majukumu yake mbayo ni makubwa na tofauti.

Hakika, Benki Kuu ya Ulaya (ECB) haikutarajia hili kuwa matokeo ya tamko lake juu ya uhuru wa benki kuu. Pengine ilidhani kuwa Mamlaka Azimio au Kamati ya Azimio ingekuwa na angalau baadhi ya uwakilishi kutoka wazoefu wa kibenki na benki kuu, na si wateule wa kisiasa.

Hiyo ndiyo imekuwa tangu Machi mwaka jana. Awali, Mamlaka ya Azimio alikuwa ikijumuisha Wizara ya Fedha na Kamisheni ya Mitaji ya Cyprus CYSEC, na pia Benki Kuu, Uwakilishi ambao ungeweza kukabiliana na nguvu kubwa za CBC. Sasa, nguvu hii ipo mikononi mwa dereva mmoja. Mamlaka na Kamati zinarundika matatizo zaidi kwa Cyprus, Sekta ya fedha, wamiliki wa ndani wa akaunti na walipa kodi, na sifa ya Jamhuri ya nje ya nchi.

Hadithi ifuatayo kwenye tovuti hii ni muendelezo wa makala hii, na inatoa orodha kamili ya vitendo vichafu na viwango vibovu vya utendaji wa Mamlaka ya Azimio ambayo yameandikwa na tovuti hii tangu sakata la FBME kuanza.