Machi 12, 2015
Makala hii inafuatia kutoka hapo juu, Mamlaka ya Azimio Yaelea Kwenye Bahari ya Matatizo.
Mamlaka ya Azimio ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) – ambayo kiukweli ni Bodi yake ya Wakurugenzi – na Kamati ya Azimio – wajumbe watatu wa Bodi hiyo – wanaonekana, bila shaka, wanawajibika kwao wenyewe na si kwa mwingine. Walivurunda kwenye Azimio la Benki ya Laiki iliyopo hapa kisiwani, na kusababisha matatizo makubwa nchini kote na wametumia tafsiri potofu ya Azimio la Amri na kulipoka tawi la Benki ya FBME. Katika mchakato huo, wamesababisha kutoaminiwa kwa kiasi kikubwa kwa Benki Kuu, kuharibu fursa ya kulinda wamiliki wa akaunti na wadai, na kuhatarisha malipo ya fidia kwa mamia ya mamilioni ya Euro.
Kwa zaidi ya nusu mwaka, tovuti hii fbmeltd.com imezungumzia matendo ya Mamlaka ya Azimio na Kamati yake ya watu watatu kwa kufanya maamuzi ya haraka yanayohusu Cyprus, sheria za kimataifa na Miongozo ya Kamati ya Basel juu ya usimamizi na vigezo bora vya kimataifa. Hapa, tunatoa muhtasari wa masuala hayo:
Julai 17, 2014 (Cyprus ilishauriwa tarehe 18 Julai) Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN alitangaza Taarifa ya Matokeo na Taarifa ya Mapendekezo ya Hatua dhidi ya Benki ya FBME kuhusu madai ya kushindwa kupambana na fedha chafu. Baada ya hapo, FBME ilikaribisha uchunguzi huru kuchunguza kitaalamu zaidi shughuli zake ambapo ilitoa majibu ya madai ya FinCEN. Majadiliano na FinCEN juu ya Ilani hiyo yanaendelea nchini Marekani.
Baada tu ya FBME kutambua madai ya FinCEN, kampuni yake tanzu ilichukua hatua za haraka na tarehe 18 Julai waliwasiliana na mshirika wake wa kisheria, Hogan Lovells, kuwakilisha maslahi ya FBME kwenye shauri la Hazina ya Marekani na kuahidi kutoa ushirikiano kamili. Siku hiyo hiyo, Benki ya FBME waliitisha mkutano na CBC kuwakaribisha kukagua shughuli zake ili kurejesha imani, hasa kwa mabenki waambata (correspondence banks) kuwahakikishia kwama tumekidhi kanuni za kupambana na fedha chafu.
Tarehe 21 Julai 2014, baada ya siku moja tu ya kudhibiti, Mamlaka ya Azimio ya CBC ilitoa amri kwa uwezo iliyokuwa nao kwenye kifungu 2A cha sheria ya Mamlaka ya Mikopo na Makampuni Mengine, ya 2013-2014, (Resolution of Credit and Other Institutions’). Lengo la Amri ilikuwa kuuza shughuli zote za tawi na kulinda wateja wa FBME. Hakuna uuzaji wowote uliofanyika na pia hakuna mteja aliyelindwa. Hakukuwa na kushauriana na wamiliki wa FBME.
Sheria hii ya Azimio ilianzishwa kwa ajili ya benki zinazofilisika au zinakabiliwa na matatizo makubwa ya ukwasi, sio kwa benki kama vile FBME ambayo ilikuwa na 104% ya ukwasi wakati huo. Hii ilimaanisha kuwa, kifedha FBME ilikuwa katika nafasi hali nzuri sana na yenye uwezo wa kulipa wateja wake wote bila shida. Kwa kutumia sharia ya Azimio isyo sahihi, Mamlaka ya Azimio ya CBC ilitumia tafsiri potofu na kulazimisha kulipoka tawi la FBME.
Kanuni ya 106 ya Muongozo wa Basel, ambao benki kuu wanahimizwa kuifuata, inasema kuwa ‘… ni wajibu wa bodi ya wakurugenzi na mameneja waandamizi wa benki, sio msimamizi, kuamua ni jinsi gani benki itatatua matatizo yake. Kwa bahati mbaya, kanuni hii ilipuuzwa na Mamlaka ya Azimio siku mbili tu za mgogoro. Uamuzi wake ulikuwa wa haraka na wenye nia mbaya, lakini pia uliashiria dhamira nyingine tofauti.
Mamlaka ya Azimio ilimteua Msimamizi Maalumu, Dinos Christofides, kuendesha tawi la FBME Cyprus kwa mabavu. Hakuna wakati ambapo alijaribu kushirikiana na wamiliki wa Benki na wakurugenzi na mara nyingi amekuwa akiwatishia mameneja na wafanyakazi kuwaachisha kazi. Alijipa majukumu zaidi ya mamlaka yake na kukwepa wajibu aliopaswa kuufanya. Aidha, wakati wa uteuzi wake alikuwa katika nafasi yenye kuashiria mgogoro, hali ambayo inaaminika bado haijatafutiwa ufumbuzi.
Walipolichukua tawi la FBME Cyprus Julai, Mamlaka ya Azimio ilifunga tawi kwa siku mbili, na kisha kwa siku mbili zaidi – kama sheria ya Azimio inavyoruhusu. Baada ya hapo, kuanzia Julai 30 tawi lilisimamishwa kufanya miamala yoyote na wateja walizuiwa kupata fedha zao mpaka Septemba 2. Hii inamaanisha kuwa tawi lilifungwa kwa siku nyingine 34 – kitendo ambacho ni kinyume na barua au sheria inavyosema.
Kitengo cha huduma za Kadi cha Benki, kililazimika kusitisha huduma tarehe 7 Agosti. Hii ni kwa sababu hakikuweza kufanya kazi bila ya kupata fedha zake zilizokuwapo FBME – matokeo ya moja kwa moja na makusudi ya maamuzi ya Mamlaka ya Azimio na Msimamizi wake. Siku nne baadaye tarehe 11 Agosti, wafanyakazi 72 wa kitengo cha huduma za kadi walipunguzwa kazi. Taarifa kutoka kwa wamiliki wa akaunti wa FBME inaonyesha kwamba idadi ya makampuni, ndani ya Cyprus na kimataifa, yamejikuta katika hali kama hiyo, kufunga shughuli na kuwaachisha kazi wafanyakazi. Hakika, hiki sicho kilichotarajiwa na Mamlaka ya Azimio.
Mamlaka ya Azimio ilikataa kuwasilisha sababu zake kwa maamuzi yake au hata kutoa mkakati wowote kuonyesha nia yake ya baadaye, hapa tunaona mgongano ulio wazi na Miongozo ya Basel au miongozo bora ya kimataifa. Ukosefu huu wa uwazi, ambao unashutumiwa sana Cyprus, ndio uliosababisha FBME Limited kuzindua tovuti hii fbmeltd.com kama njia kukidhi mahitaji ya habari. Zaidi ya kompyuta za watu 60,000 zimetumika mara kwa mara kutafuta taarifa. Tarehe 5 Septemba tovuti hii ilishambuliwa na kunyimwa ruhusa ya kutoa habari na kufungwa. Ndani ya masaa 48 iliibuka tena nje ya mipaka ya Cyprus.
Kumekuwa na sintofahamu kubwa kimataifa. Tarehe 19 Agosti, Fitch Ratings ilitoa ripoti inayoelezea wasiwasi wake wa matumizi ya Azimio dhidi ya tawi la benki ya kigeni. CBC na Mamlaka yake ya Azimio hazikujaribu kuratibu maamuzi yake kwa kushirikisha Msimamizi wa Makao Makuu ya FBME, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), licha ya mapendekezo yaliyopo katika Mwongozo wa Basel.
Msimamizi aliyeteuliwa na Mamlaka ya Azimio alitangaza Septemba 1 kwamba kuanzia siku inayofuata angeweza kuruhusu miamala kwa kiasi kidogo kuanza. Hii ilisababisha usumbufu mkubwa ambapo wateja wa FBME walitakiwa kuja wenyewe hadi Cyprus ili kuhudumiwa kwenye akaunti zao. Hajatoa maelezo kwa nini akaunti 300 zimefungiwa, licha ya sheria inayosema kwamba wateja walio kwenye kundi moja wanapaswa kupewa huduma sawa. Akaunti zilizofungiwa zilifunguliwa Novemba 6 bila ya maelezo.
Kwa idhini ya Mamlaka ya Azimio, Msimamizi aliendelea kutoa maamuzi ambayo yamesababisha madhara ya wazi kwa FBME na wateja wake. Inashangaza, wakati wa uteuzi wake Msimamizi aliandika kuwa moja ya malengo yake ilikuwa kulinda maslahi ya wateja! Tunashangaa jinsi gani anaweza kulielezea hili ukiangalia matendo yaliofuatia.
Maswali yalianza kuulizwa kuhusu Mamlaka ya Azimio katika vikao vyote ndani na nje ya nchi. Baraza la Wawakilishi la Cyprus lilianza kuchunguza suala hili na lilimepangwa kusikilizwa katika Bunge Februari 17. Usikilizwaji uliahirishwa baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuingilia kati, ingawa iliwekwa wazi kwamba viongozi waliohusika “… bado wataitwa kujibu hoja za matendo yao, kutokuchukua hatua au uzembe mwingine”.
Usuluhishi katika Mahakama ya ICC mjini Paris chini ya Mkataba wa ulinzi wa ushirikiano wa uwekezaji kati ya Lebanon / Cyprus ilianza tarehe 28 Oktoba. Maelekezo yake ya kwanza ilikuwa kuweka kusimamisha hatua zote zilizotaka kuchukuliwa na Mamlaka ya Azimio ikiwa ni pamoja na kutochukua fedha za FBME na kutouza tawi lake.
Kisha tarehe 31 Oktoba, ilifahamika kwamba Chrystalla Geordhadji, Gavana wa CBC, alituhumiwa kuhusu suala la mikataba wake wa kazi na mgongano wa kimaslahi katika kesi ya kisheria dhidi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Laiki, Andreas Vgenopoulos. Kwa sasa anachunguzwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu katika kwenye suala la hili la pili.
Katika kuhoji tabia na utaalamu wake, mbunge mmoja aliuliza kwa nini yeye na Mamlaka ya Azimio ameruhusiwa kupotosha swala la FBME ambapo anaweza kusababisha gharama kwa Jamhuri ya mamia kwa mamilioni ya Euro kama fidia.
Wakikabiliwa na ukosefu wa uwazi kwenye Mamlaka ya Azimio, wamiliki wa FBME walitangaza tarehe 2 Novemba kwamba watawawajibisha maofisa waandamizi wa CBC kwa hasara wanayoisababishia Benki na kampuni yake tanzu. Tovuti ikuwa ikifuatilia kwa karibu suala hili lililosababishwa uzembe wa Mamlaka ya Azimio, na ukosefu wake wa kuzingatia sheria na vigezo bora vya kimataifa, na kutokuwa na nia ya kueleza kilicho nyuma ya vitendo vyake au jinsi inavyotarajia kutatuwa jambo hili. Walijichimbia wenyewe ndani ya shimo Julai 2014. Katika kujaribu kujitoa nje tangu wakati huo, ndio wanajichimbia zaidi ili wao na watu wa Cyprus waingie kwenye matatizo makubwa zaidi.
Katika matukio matano tofauti kati ya Juni na Novemba Mamlaka ya Azimio ilituma timu ya wafanyakazi ya CBC na wahasibu wa PwC kuichunguza FBME tawi la Cyprus. Hakuna hata wakati mmojaambapo matokeo yamewekwa hadharani au kuyakabidhi kwa FBME.
Akijibu shutuma kutoka kwa mmoja wa wajumbe wake wa bodi, CBC ilitangaza nia yake ya kufanya utafiti mkubwa kwa shughuli zake zote kwa lengo la kuleta “Mabadiliko na Utendaji wa Kisasa” Huenda hii itaangalia pia utendaji kazi wa Mamlaka ya Azimio na Kamati yake, na hatua za kusimamia shughuli zake.
Mjumbe wa bodi ya CBC mhusika, Stavros Zenios, alionyesha kutoridhika kwake na Wasimamizi Waandamizi ndani ya CBC ambao wanaonekana kutopenda mabadiliko. Alihusisha ripoti ya waangalizi wa kimataifa ambayo ilionyesha udhaifu mkubwa uliochangia kuanguka kwa sekta ya kibenki ya Cyprus mwaka 2013, na kuonya kuwa wangeweza kusababisha janga jingine. Mamlaka ya Azimio haiwajibiki kwa mtu yeyote bali kwa yenyewe na inaonekana kuwa katika ‘moyo’ wa matatizo.
Ukosefu wa utaalamu na uzoefu ni tatizo la wazi. Gavana, ambaye alikuwa amefanya kazi miezi michache tu wakati Azimio la Amri lilipotolewa dhidi ya FBME, alikuwa hajawahi kufanya kazi katika aidha benki kuu au benki kabla ya hapo. Wakurugenzi wawili Watendaji wanaounda Kamati ya Azimio na Gavana, ni wachumi na wasomi, na na hawana uzoefu wa kutosha. Ni sawa sawa na kipofu kumuongoza kipofu.Kwamba wameruhusiwa kushiriki katika maamuzi yanayoisababishia Jamhuri hasara kubwa na idadi kubwa ya watu kupoteza maisha yao na akiba, ni kashfa kubwa ya kitaifa. Hatua za haraka zinahitajika ili jeraha hili liweze kupona.