Wapili ajiuzulu kutoka Bodi ya CBC

Machi 20, 2015

 Stavros Zenios, mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Cyprus, alijiuzulu kutoka Bodi asubuhi hii ya Machi 20. Yeye ni mwanachama wa pili kuachia nafasi hizo katika siku za karibuni, Stelios Kiliaris alijiuzulu wiki iliyopita akitoa maelezo kuwa haiwezekani kuendelea kutumikia mamlaka hiyo katika mazingira ya sasa. Bw Kiliaris pia alikuwa mmoja kati ya wanachama watatu wa kamati walioiwekea FBME azimio la masharti.

Kwa kujielezea kwa waandishi wa habari kuhusu kujiuzulu kwake, Stavros Zenios alitoa taarifa na sababu za uamuzi wake, ambao pia ameziweka kwenye mtandao wa Kigiriki katika blogu yake: https://zenios.wordpress.com

Ametoa sababu saba ambazo zimesababisha uamuzi wake. Miongoni mwa hizo, ya tano, ikisema kwamba yeye aliamua kujiuzulu kutoka Bodi ya Wakurugenzi kwa sababu ya kukataliwa mapendekezo yake ya kimaandishi ya Julai 28, 2014 ya kwamba uchunguzi wa ndani ufanyike katika kesi ya FBME na mbinu zilizochukuliwa na Gavana akishirikiana na Wakurugenzi Watendaji wawili.