Januari 23, 2015
Tarehe 21 Januari, mkutano ulifanyika jijini Washington DC kati ya wawakilishi wa Benki ya FBME na Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN. Lengo lilikuwa kujadili zaidi Notisi ya Matokeo ya FinCEN (NOF) na Ilani ya Mapendekezo (NPRM), iliyochapishwa kwenye Daftari la Shirikisho tarehe 22 Julai 2014, na majibu ya Benki ya FBME ya masuala yaliyoorodheshwa kwenye Notisi hizo.
Majibu ya Benki ya FBME, ambayo ni mamia ya kurasa za ripoti ya utafiti na nyaraka nyingine, yalitokana (kwa sehemu kubwa) na uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na EY (Ernst and Young) na kampuni ya kisheria ya kimataifa ya Hogan Lovells. Maoni hayo ya Umma, yaliyochapishwa na Hogan Lovells mwezi Septemba, yanapatikana hapa.
Hogan Lovells walichunguza na kutoa majibu ya kina kwa masuala yaliyotolewa kwenye notisi hizo. Ripoti hiyo ina taarifa kuhusu dhamira ya FBME ya kutekeleza taratibu zote za Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na jaribio lake la kushiriki katika mjadala na CBC wakati Benki ilipopinga kilichoonekana kama madai yasiyo na haki yaliyowekwa dhidi yake na mdhibiti (CBC ).
Kwa upande wake, EY walifanya uchunguzi huru kwa Benki ya FBME na sera zake za kupambana na fedha chafu na taratibu za uendeshaji, na miamala maalum iliyotambuliwa katika Ilani ya Matokeo ya FinCEN. Kama EY walivyoona kwenye tathmini yao, sera za “AML (kupambana na pesa chafu) za FBME zinakidhi matakwa ya Maelekezo ya Benki Kuu ya Ulaya (EU) na Benki Kuu ya Cyprus.
Hata hivyo, Hogan Lovells na EY walitoa mapendekezo katika baadhi ya maeneo ambapo sera za FBME zinaweza kuboreshwa na mkutano huo ulitoa fursa ya kuonyesha utekelezaji wa mapendekezo hayo. Aidha, uchunguzi wa Hogan Lovell na EY uionyesha kwamba madai mengi kwenye Ilani ya Matokeo hayakuwa sahihi, yaliacha taarifa muhimu pia hawakuzingatia hatua za marekebisho zilizochukuliwa na FBME, au ni kauli za jumla kuhusu hatari ambayo imepunguzwa makali kwa kuimarishwa hatua za juu kukabiliana na hatari hizo. Kwa msingi huu, Benki ya FBME, kwa heshima kubwa iliomba kwamba Ilani ya Matokeo na Mapendekezo (NPRM) ziondolewe na kusisitiza kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa FBME haikufanya chochote kibaya.
Benki ya FBME imekaribisha fursa hii ili kuendelea kubadilishana taarifa na FinCEN na inathibitisha nia yake ya kufanya kazi kwa kushirikiana na FinCEN, ili FBME na wateja wake waweze kurudi kwenye shughuli zao za biashara haraka iwezekanavyo.