Ufunguzi wa Tawi – kiana!

Oktoba 20 2014

Tawi la Cyprus la benki ya FBME limefunguliwa leo asubuhi baada ya kurudi ofisini msimamizi wa tawi hilo ambae aliteuliwa na benki Kuu ya Cyprus. Kama tulivyo wapa habari, tawi hilo lilizuiwa na Msimamizi huyo kuendelea na shughuli zake za kawaida wiki iliopita, wakati alipokuwa anaenda likizo.

Kwa sasa amerudi ila ni matarajio kuwa ataruhusu biashara iendelee kama awali: yaani ataruhusu wateja wenye maombi kwenye tawi la Cyprus kuendelea kuchukua fedha kwa kiwango hadi kufikia EUR 10,000 kwa siku. Wateja walio nje ya nchi na ambao hawana wawakilishi mjini Cyprus bado hawata ruhusiwa. Kuna walio wengi akaunti zao zimezuiwa kwa amri ya Msimamizi (ambae bado hajatoa sababu ya zuio hilo). Ndio maana tunasema ni ufunguzi wa kiaina! Kwa kuwa alikuwa na mapumziko ya wiki moja, tunadhani amepata muda wa kufikiria kujibu maswali aliopewa mwezi uliopita. Tutarudi kwenye hayo maswali tena.