Oktoba 22 2014
FBME Limited imeanza tena juhudi za kupigana ila kuweza kuzuia uuzwaji wa tawi la Cyprus uliopangwa na Benki Kuu ya Cyprus.
Kampuni hii tanzu, ilitoa tamko lake hilo siku ya kwanza (Oktoba 21) iliopangwa kusikilizwa kesi kwenye mahakama ya wilaya ya Nicosia, ambapo iliweka zuio la kutouza tawi la FBME Benki ya Cyprus. Kesi inaendelea.
FBME Limited ina pinga vikali uuzaji wa tawi hilo, na inaona ni amri hatarishi na isiyokuwa na hoja yeyote ya kisheria. “Benki Kuu ya Cyprus inabidi isubiri mpaka itakaposikilizwa kasi ya malalamiko kwenye shauri la msingi kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi huko mjini Paris, ambayo itasikilizwa hivi karibuni,” imesema tamko hilo. Benki Kuu ya Cyprus ilitoa amri ya uuzaji wa tawi hilo sambamba na hatua za kuwekea vikwazo mnamo tarehe 21 Julai 2014. Hatua hizo zinakiuka makubaliano ya ya kisheria yaliosainiwa tarehe 5 Juni 2002 baina ya Lebanese-Cyprus (sheria namba 399) kifungu ambacho kinazuia uuzaji ama utaifishwaji wa mali za wananchi wa nchi mojawapo. Ibara namba 12 ya makubaliano hayo inasema wazi kuwa katika mtafaruku wowote utakaotokea pande zote zichukue zichukue hatua zitakazokubalika na wahusika wote za kisulihishi.
FBME Limited inaona kwamba, Benki Kuu ya Cyprus imeweka na kukiuka sheria zake kwa kutimiza azma yake ya kuiwekea vikwazo benki hii, hatua ambayo inatakiwa ichukuliwe kwa benki ambazo zinakabiliwa na kufilisika. FBME inasema Tamko hili limetumika kwa madhumuni ya kuwaumiza wateja na kuharibu sifa ya Benki. Hatua pia imesababisha kusimamishwa kwa shughuli za idara katika kitengo cha kadi na kusimamishwa kazi wafanyakazi 75 wa idara hiyo. Azimio hilo limewekwa na Benki Kuu bila kushirikisha msimamizi wa nyumbani Benki Kuu ya Tanzania.
Hatua hizi za benki kuu ya Cyprus zilichukuliwa baada ya FBME kutuhumiwa kuhusika na upitishwaji wa fedha chafu na idara ya hazina ya marekani FinCEN iliotoa tarehe 17 Julai 2014. FBME Benk ilipewa muda hadi tarehe 22 Septemba kujibu tuhuma hizo, hatua ambayo FBME Benki imeshafanya na nakala ya majibu haya pamoja na maoni ya wananchi inapatikana katika mtandao wetu chini ya kichwa kisemacho “yanayotuhusu” FinCEN inaendelea kusoma majibu ya Benki ya FBME na inategemewa kutoa uamuzi wake katika wiki zijazo. FBME Limited inaamini kuwa uamuzi wa kuendelea kuuza tawi hilo la Cyrus inavunja uwezo wa FinCEN kutoa uamuzi sahihi. Kwa kuongezea, FBME inaamini kuwa hatua hizo za Benki Kuu ya Cyprus ni hatarishi kwa mji wa Cyprus na unaharibu sifa kama wakala wa kimataifa wa kiabiashara na italeta hatua zaidi za kisheria zichukuliwe na kusikilizwa katika mahakama za hapo na kimataifa.