Sakata ilipofikia sasa

14 Oktoba 2014

Baada ya uchunguzi makini katika shughuli zake, FBME imeweza kuwasilisha majibu kwa FinCen, ofisi ya hazina Marekani, tunafahamu kuwa sasa ripoti hiyo inasomwa kwa umakini na kufikiriwa. Nakala ya maoni ya Umma ambayo iliwasilishwa pamoja ipo hapa.


Ripoti hiyo ya FBME iliwasilishwa tarehe 22 Septemba kutokana na taratibu zilizowekwa, ikiwapa ofisi hiyo ya FinCEN muda maalum kusoma majibu hayo na kutoa uamuzi unaostahili. FBME Benki kwa heshima imeiomba taarifa ya matukio na mapendekezo ya FinCEN yaondolewe. Nakala ya matukio ya sasa yanaweza kupatikana hapa.

Kitu ambacho kitakuwa bado hakijafikiwa uamuzi ni uendeshwaji uendavyo wa FBME tawi la Cyprus, kama alivyoelezea mtangazaji mmoja wa kimarekani. Pamoja na mpango wa kwanza kuwepo – imekuwepo mipango mingi ambayo imeambatana na hii – haijaenda vizuri kwa Benki Kuu ya Cyprus. Wameishi kwenye mkanganyiko, ulioharibu sifa ya nchi, wamekuwa ndio sababu ya watu kuachishwa kazi na kusababisha madhara kwa wateja, wafanyakazi na Benki yenyewe. Haiyumkiniki kuwa wanataka kutoka katika hali hii ila “wameshikwa na chui kwenye mkia”, na inabidi watafute njia ya kujinasua.