Kesi ya Mahakama ya Wilaya kusikilizwa Oktoba 21

Septemba 30, 2014

Tarehe 29 Septemba, Mahakama ya Wilaya ya Nicosia ilipanga maombi ya muda yaliowasilishwa na wabia wa FBME Bank kwa ajili ya kusikilizwa tarehe 21 Oktoba 2014.

Kama sehemu ya utaratibu wa maombi hayo, wanahisa wa FBME Bank Limited, waliwasilisha maombi hayo tarehe 14 Agosti 2014, ili kusaidia yatakayo kuja katika usuluhishi wa kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara mjini Paris, ambayo wanahisa wanaomba haki za mikataba na mwekezaji zieleweke baina ya nchi ya uwekezaji  kati ya Lebanon na Cyprus iliosainiwa mwaka 2002.

Ilithibitika na kusisitizwa kuwa ahadi ya kutokutoa amri ama kuweka makubaliano ya uuzaji wa tawi baina ya Benki Kuu ya Cyprus na Mamlaka yenye Azimio, mpaka hukumu ya maombi ya mpito ipite.