FBME Bank yawasilisha taarifa yake kwa FinCEN

Septemba 23, 2014

Uwasilishwaji wa ripoti kwa Idara ya Hazina ya FinCEN ofisi ya Washington DC Marekani unaendelea. Hii ni kwa mujibu wa kipindi cha siku 60 kilichoruhusiwa kwa ajili ya kukabiliana na ilani ya FinCEN ya kutafuta na taarifa ya mapendekezo iliyotolewa mwezi Julai.

Taarifa ya kurasa 28 kwa umma imewasilishwa kwa niaba ya Benki na wanasheria wake wa kimataifa Hogan Lovells. Nakala ya taarifa hii ni inapatikana hapa.

Taarifa hiyo imetoa kauli ya wazi kwamba wahasibu wa Ernst and Young, wamechunguza kwa kina na wametathmini ya kuwa FBME inafuata mpango na taratibu zinazostahili na vilevile “inashirikisha mahitaji” ya tatu ya EU kuhusu maelekezo ya fedha chafu na maelekezo ya nne ya Benki Kuu ya Cyprus kwa taasisi za mikopo kwa mujibu wa Ibara 59 (4) ya taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Fedha chafu ya mwaka 2007 hadi 2013.

Taarifa hiyo inaendelea kutoa kauli kuwa, ‘Tathmini EY ina taarifa kwamba FBME ina “itifaki zinazotakiwa kuruhusu Benki kuendelea na Programu iliyo na mahitaji ya kisheria”.’

FBME imeendelea kukasisitiza ahadi yake ya kushirikiana na serikali ya Marekani, Cyprus na Tanzania katika mapambano dhidi ya fedha chafu na ufadhili wa ugaidi. Mapendekezo yamefanywa katika maeneo kadhaa ambapo inaweza kuboreshwa; Benki  tayari imeshaanza kutekeleza.