Juni 10, 2015
Wakati mvutano ukiendelea kuhusu utendaji wa viongozi waandamizi wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC), imependekezwa kwa mara nyingine tena kwamba taasisi hii lazima iwapime wakurugenzi wake na uongozi mzima.
Juni 10, 2015
Wakati mvutano ukiendelea kuhusu utendaji wa viongozi waandamizi wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC), imependekezwa kwa mara nyingine tena kwamba taasisi hii lazima iwapime wakurugenzi wake na uongozi mzima.
Mei 25, 2015
Maamuzi ya hivi karibuni kwenye mchakato wa usuluhishi katika Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris yamekaribishwa na wamiliki wa FBME Limited. Wameeleza dhamira yao ya kutoa ushirikiano kamili kwa maamuzi ya mahakama hiyo na kufikia ufumbuzi wa mzozo kwa kushirikiana na washtakiwa.
Mei 21, 2015
Taarifa kwa vyombo vya habari imetolewa kuhusiana na hatua ya hivi karibuni ya Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris. Hii inahusiana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya hivi karibuni na inaweza kusomwa kwa kubonyeza hapa.
Mei 18, 2015
Dinos Christofides, mhasibu aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC), kuiendesha Benki ya FBME tawi la Cyprus ameacha ghafla jukumu lake hilo Ijumaa Mei 15 mwaka 2015. CBC alitangaza kwenye tovuti yake kwamba Mr Christofides amejiuzulu kwa sababu za kibinafsi, ingawa katika mazungumzo mengine alitoa mtazamo tofauti.
9 Mei 2015
Tarehe 21 Julai, 2014 mnamo saa 5 usiku, Benki Kuu ya Cyprus ilitangaza kuanza kwa hatua ya Azimio kwa tawi la benki ya FBME la Cyprus. Kama tujuavyo, Azimio ni njia inayotumika kwa uendeshaji wa shughuli zote za benki inayofilisika, lakini haijatumika kwa benki iliyo na fedha, yenye ukwasi wa kutosha kama FBME tawi la Cyprus. Katika kuifikia hatua hii, Benki Kuu ilishindwa kuratibu – au hata kuijulisha – Benki Kuu ya Tanzania ambayo ni Msimamizi Mkuu wa Makao Makuu ya Benki ya FBME. Kuanzia siku hiyo hadi sasa, CBC imeshindwa kuunganisha matendo yake na yale ya mamlaka kuu nchini Tanzania au hata kufuata kanuni na sheria za Cyprus na Umoja wa Ulaya (EU).
Mei 5, 2015
Ukweli wa mambo umeibuka kutokana na maelezo ya uteuzi wa msimamizi wa pili wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kuendesha tawi la Benki ya FBME la Cyprus. Wasimamizi hawa wawili wanalipwa zaidi ya mishahara (kwa pamoja) ya Gavana wa CBC na mtu anayemtambua kama bosi wake, Rais wa Benki Kuu ya Ulaya – ECB, Mario Draghi. Pengine unaweza pia kuunganisha mishahara ya wafanyakazi wengine wa Bodi ya Wakurugenzi ya CBC na bado ukabaki na chenji.
3 May 2015
Taarifa za hivi karibuni zilieleza kimakosa kuwa wafanyakazi wa FBME wamekwenda Polisi na Benki Kuu ya Cyprus kupeleka madai yasioeleweka kuhusiana na ukiukwaji wa mfumo wa kupambana na pesa chafu. Ukweli ambao FBME inauelewa ni kwamba, watu wanaozungumziwa ni watu binafsi wanaohusishwa na makampuni ya Uingereza ambayo kwa sasa wako katika madai na FBME kuhusu mgogoro wa ankara zilizokataliwa na huduma.
Aprili 30, 2015
Benki Kuu ya Cyprus (CBC) imewateua wachunguzi wapya ili kukagua mifumo ya kupambana na fedha chafu kwenye tawi la FBME Cyprus. Washauri walioteuliwa na Benki Kuu ni kampuni ya sheria ya kimataifa ya DLA Piper, wachunguzi wa fedha Kroll na wanasheria wa Cyprus Georgiades & Pelides.
Aprili 16, 2015
Mnamo tarehe 9 April, 2015, FinCEN, taasisi ya uchunguzi ya Hazina ya Marekani, ilitoa makala ya uthibitisho kuwa walikutana na wanasheria wa FBME Hogan Lovells mjini Washington DC.
Kama unahitaji kuona hilo tangazo na maelezo ya FBME bonyeza hapa.
Aprili 2, 2015
Viongozi waandamizi wa serikali, ikiwa ni pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Cyprus, walishindwa kuhudhuria mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 31 Machi wa Kamati ya Usimamizi ya Baraza la Cyprus. Mkutano huu ilikuwa na lengo la kuruhusu Wabunge kuchunguza sababu na matokeo ya hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu dhidi ya Benki ya FBME tawi la Cyprus na athari za vitendo hivi juu ya maslahi ya umma nchini Cyprus. Mkutano umepangwa tena tarehe 21 Aprili na kwamba utafanyika kwenye kamera.