Novemba 20, 2014
Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Meneja Msimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania na Benki ya FBME Dar Es Salaam, FBME Limited inachukua hatua za kupata ukwasi wa ziada kwenye tawi la FBME Cyprus. Hii inafanywa ili kuhakikisha uwepo wa amana ya kutosha kwa wateja kuepuka tatizo la kiwango cha siku cha muamala kilichowekwa na msimamizi aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus.