Author Archives: Editor1

Mahakama ya Wilaya ya Marekani Yaweka Zuio la Mwanzo dhidi ya FinCEN na Maamuzi yake ya Mwisho.

Agosti 28, 2015

Mnamo Agosti 27, Mahakama ya  Wilaya ya Columbia, wamekubali kuweka pingamizi la awali dhidi ya FinCEN na washitakiwa wengine wa Marekani na kuzuia Maamuzi ya Mwisho ya FinCEN yasifanye kazi hadi hapo Mahakama itakapotoa humumu yake ya mwisho, kama ilivyoombwa na FBME Limited na  Benki ya FBME Limited. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye amri ya mahakama kwakubofya hapa.

Continue reading

Uamuzi wa FinCEN Una Makosa Mengi ya Ukweli na Kisheria

Julai 27 2015

 FBME Limited imeisoma hukumu ya mwisho ya Taasisi ya Kuangalia Makosa ya Kifedha ya Idara ya Hazina ya Mrekani (FinCEN)  iliyotolewa tarehe 23 Julai 2015, na kutoa taarifa ifuatayo:

Uamuzi wa FinCEN hauwezi kuachwa kukosolewa. Ingawaje Benki na washauri wake walifanya juhudi kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuelezea mifumo ya kupambana na fedha chafu AML na uendeshaji,  miamala na shughuli nyingine, makosa makubwa ya kisheria na upotoshaji wa ukweli yaliyomo kwenye hukumu hiyo ya mwisho inaonyesha kwamba iliandikwa na watu bila kutilia maanani maelezo muhimu tuliyowapelekea sambamba na nyaraka nyingine walizokwisha kuwa nazo.

Benki inakusudia kutafuta njia yoyote inayowezekana kujilinda ipasavyo dhidi ya udhalimi huu kwa kufungua kesi kwenye mahakama ya Washington DC dhidi ya Idara ya Hazina ya Marekani.

Taarifa zaidi zitatolewa katika wakati muafaka kupitia tuvuti hii ya www.fbmeltd.com

 

 

 

 

Kila Mmoja Anaathirika na Sakata hili

19 Julai 2015

Tarehe 17 Julai 2014, mlolongo wa matendo ulianzishwa ambao ulikuwa na madhara makubwa kwa wateja, wafanyakazi na washirika wa Benki ya FBME, ndani na nje ya nchi. Watu wamepoteza kazi zao na makampuni yamefungwa. Aidha, kuna waathirika wengine ambao wameanza kuhisi athari kwa sasa – walipa kodi, serikali, mamlaka ya benki na mfumo wa haki wa kisiwa cha Cyprus. Katika ujumbe huu, Benki ya FBME inatoa maoni yake juu ya nini kimetokea.

Continue reading

FBME Yaiumiza Vichwa CBC

Juni 16, 2015

Miezi kumi na moja baada ya uamuzi usiokuwa wa kawaida wa CBC wa kuchukuwa operesheni za FBME nchini Cyprus, wasiwasi wa umma unamiminika huku vyombo vya habari nchini vikionyesha kuwepo wasiwasi huo. Gazeti la kila wiki kisiwani Cyprus, linalochapishwa kwa Kiingereza limeandika makala ifuatayo:

Continue reading

Plus ça change, plus c’est la meme chose*

Juni 11, 2015

(*Mabadiliko Yanapozidi, Mambo Hubakia Kama Yalivyo)

Barua kutoka kampuni ya sheria Limassol na kutumwa kwa wafanyakazi wa FBME kwa niaba ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) na msimamizi wake kuwakumbusha wafanyakazi juu ya wajibu wao wasishiriki kwenye utoaji wa taarifa kwa vyombo vya habari na hasa kwa tovuti flani (inaweza kuwa tovuti yoyote). Kwa kweli inaeleza kuwa utoaji habari huo ni ‘uvujishaji’, taarifa ambao ni sawa na ‘Watergate’ au mapambano dhidi ya utawala wa kiimla.

Continue reading