Author Archives: Editor1

Kazi Nzuri Sana – Kama Unaweza Kuipata!

Februari 25, 2015

Kuendelea na mlolongo wa matamko, Msimamizi wa Benki Kuu, Dinos Christofides, ametoa tamko kwa mameneja na wafanyakazi wa FBME tawi la Cyprus kuwakumbusha kwamba muda wa kawaida wa kufanya kazi tawini kwa siku ni 2:30-11:00. Pia aliongeza kuwa mfanyakazi mwandamizi yoyote anyetaka kwenda likizo anatakiwa kupeleka maombi yake kwenye idara ya Wafanyakazi na kubiri kupata kibali cha Mr Christofides .

Continue reading

Je, Fedha za FBME zinaweza kutumiwa vibaya kwa Bima ya Amana?

Februari 10, 2015

Habari zisizo rasmi zinasikika kuwa Benki Kuu ya Cyprus inatarajia kutumia kwa ubadhirifu fedha za FBME Benki kwa ajili ya malipo yanayohusiana na ulinzi wa amana ya bima, kitu ambacho kwa uhakika itaifanya Benki ilipe mara mbili. Hii haiwezi kuwa ni nia ya Benki Kuu, kwa kuwa inajua vizuri kwamba hakuna msingi wa kisheria kwa ajili ya kuchukua hatua hiyo.

Continue reading

Maswali yaibuka Bungeni Cyprus

Februari 12, 2015

Kama ilivyoonekana kwenye tovuti ya Bunge la Cyprus leo (http://www.parliament.cy/easyconsole.cfm/id/326): Baraza la Wawakilishi limeitisha mkutano ili kuendelea na uchunguzi wake katika hatua zilizochukuliwa na Benki Kuu dhidi ya FBME Bank ‘ambayo inaweza kuleta matokeo yenye maslahi ya umma’. Mkutano huo, utakaofanyika saa 09:20 siku ya Jumanne, tarehe 17 Februari, utakuwa chini ya wenyeji wa kamati ya bunge ya Mtetezi (Ombudsman). Jina halisi ya kamati hii ni Taasisi ya Kiutamaduni na Kamishna wa Utawala (Ombudsman). Kazi ya kamati hii ni usimamizi wa uendeshaji wa vyombo vya umma na taasisi.
Continue reading

Malalamiko ya Ushindani yaanza

Februari 14, 2014

Hoja zimeanza kufumuka na zimewasilishwa katika vikao vya Tume ya Ushindani ya Cyprus katika suala la malalamiko dhidi ya kampuni ya JCC Payments Systems Limited, wanahisa wake na mabenki mengine katika suala kwa utoaji wa kadi za malipo na huduma zake. Kesi itasikilizwa tena Jumatatu, Februari 16.

Miongozo ya Basel yaipa Mabenki Kuu Njia Bora

Februari 16, 2015

Miongozo ya Basel ni miongozo ya kina yenye mapendekezo yaliyotolewa kwa ajili ya mabenki makuu ili kuwasaidia katika kukabiliana na taasisi zilizo chini ya usimamizi wao ambazo zinakabiliwa na matatizo. Kamati ya Basel ilichapisha miongozo hiyo mwaka 2002 kwa ajili ya Usimamzii wa Mabenki na kurekebishwa mwaka 2014. Makala hii inaangalia thamani ya matumizi ya hiyo miongozo.
Continue reading

Kitengo cha Huduma za Kadi Cha FBMEKufungua Malalamiko ya Ushindani

Februari 6, 2015

Usikilizwaji wa kesi ya malalamiko ulioanzishwa na Tume ya Ushindani ya Cyprus utaanza wiki ya mwanzo ya Februari 9 na inatarajiwa itafikia mwisho mwezi Machi. Hii inahusiana na matokeo ya uchunguzi ya Tume dhidi ya JCC Payment Systems Limited, wanahisa wake na benki nyingine zinazohusiana hasa na utoaji wa kadi za malipo na kuendesha huduma za malipo kwa kadi. Malalamiko yanahusiana na suala la kutumia hali ya msimamo wa kuzuia ushindani na kuvunja sheria ya Ushindani namba 3 na 6 ya Cyprus na Sheria namba 101 na 102 ya Mkataba wa Umoja wa Ulaya.
Continue reading

Tovuti Yaeneza Habari

Januari 30, 2015

Wakati wa mwisho wa miezi minne ya mwaka 2014, watu kutoka nchi 144 alitembelea tovuti hii, fbmeltd.com, karibia watumiaji maalum 58,000, huingia takriban mara 600,000. Hii inahusisha kipindi cha kuanzia Septemba 7, 2014 wakati tovuti ilipoanzishwa na baada ya kupatwa na mshtuko wa ‘kuingiliwa’, hadi mwisho wa mwaka. Kipindi cha awali kabla ya kushambuliwa, kutoka muda wa uzinduzi katikati ya Agosti hadi mwanzoni mwa Septemba, inaonekana kuwavutia wengi hadi kufikia watumiaji 100,000.
Continue reading

Mafunzo ya Kuzuia Utakatisishaji wa Fedha haramu na Kufadhili Ugaidi (AML na CTF)

Januari 23, 2015

Kama sehemu ya ahadi yake kwa FinCEN, Benki ya FBME itafanya upya mafunzo kwa wafanyakazi ili kuonyesha ahadi yake ya utekelezaji wa udhibiti wa mifumo ya benki wakati wote. Mafunzo haya mapya yataongeza elimu ambayo tayari wafanyakazi wanayo na itazidisha mifumo ya udhibiti wa Benki. Lengo hasa ni sera ya kukabiliana na kupambana na fedha haramu, jua-mteja-wako, kukabiliana na kufadhili ugaidi na vikwazo vya kiuchumi.

Continue reading

Jopo la Usuluhishi ICC Laundwa

Januari 26, 2015

 Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Biashara  mjini Paris imekubaliana juu ya uteuzi wa jopo la wasuluhishi walioteuliwa na wamiliki wa Benki ya FBME, Jamhuri ya Cyprus na mwenyekiti wa mahakama. Moja ya kazi ya kwanza kwa wasuluhishi hao ni kuangalia kwa haraka suala la madhara yaliyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na msimamizi wa Benki Kuu ya Cyprus kufuatia kukubaliwa kwa shauri la usuluhishi na ICC tarehe 28 Oktoba 2014.

Continue reading