Category Archives: Uncategorized @sw

Jaji wa Marekani Aamuru Subirisho

22 July 2016

Julai 22, 2016, Jaji Cooper wa Mahakama ya Wilaya ya Columbia, Marekani ameamuru “kwamba utekelezaji wa hukumu ya mwisho [kuiwekea vikwazo Benki ya FBME] isubiri hadi hapo Mahakama hii itakapotangaza tena.” Kwa hiyo, hukumu ya hivi karibuni ya FinCEN haitafanya kazi wakati pande zote zikisubiri maelekezo zaidi kutoka Mahakama hiyo. Nakala ya suburisho II ya Jaji Cooper iemambatanishwa hapa.

.

Usawa Kwenye Sheria? Sio kwa CBC au FinCEN

Julai 20, 2016

Mwishoni mwa wiki iliyopita ilitangazwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kwamba Benki ya Hellenic, taasisi ya fedha iliyosajiliwa katika Jamhuri ya Cyprus, walikiuka sheria ya kupambana na fedha chafu na kufadhili magaidi, na wajibu wa ‘kumjua-mteja wako’. Mapungufu haya au udhaifu, CBC imesema, yameonekana “… kwenye ukaguzi wa ndani uliofanywa Septemba 2014, kuchunguza shughuli za Benki ya Hellenic katika miaka iliyotangulia.”

Continue reading

Tahadhari ya Uzzaji wa Mali

Juni 25, 2016

FBME Limited, kampuni ya tanzu ya Benki ya FBME (“Benki”), imegundua kwamba Msimamizi Maalum aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) anajaribu kuuza mali ambazo ni mali ya Benki. Jitihada za kuuza mali za Benki zinafanyika bila taarifa au ridhaa ya Meneja wa Kisheria wa Benki Kuu ta Tanzania ambaye ndio mdhibiti mkuu.

Continue reading

Uamuzi wa Mahakama ya Utawala Waonekana Kutokuwa Sahihi

Mei 27, 2016

Maamuzi ya Mahakama ya Kiutawala ya Cyprus kukataa maombi ya Benki ya FBME kuahirisha hatua iliyopangwa ya Benki Kuu ya Cyprus ya kufuta leseni ya tawi ka FBME imetangazwa kuwa hayana mashiko. Maombi ya awali yalifanywa takriban miezi 21 iliyopita kwenye Mahakama Kuu ya Cyprus, na yalikuwa ni maombi kwa ajili ya hukumu ya mpito. Mahakama ya Utawala iliisikiliza kesi hiyo ili kupunguza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama Kuu, na inajulikana kwamba Mahakama ya Utawala haina kawaida ya kutoa maamuzi ya mpito.

Continue reading

Ombi la CBC la Kutaka Maelezo Binafsi ni Kinyume cha Sheria

Mei 24, 2016

Mawasiliano ya hivi karibuni kutoka Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kwenda kwa wamiliki wa akaunti wa tawi la Benki ya FBME Cyprus ni kinyume cha sheria na inapingana na maamuzi yoyote ya kisheria ya huko nyuma, FBME imesema. Mawasiliano hayo, yaliyoitwa na CBC “maelezo ya mwenye akaunti ‘”, yanawataka wamiliki wa akaunti kuwasilisha maelezo yao binafsi na ni mbinu ya mlango wa nyuma ya kuwafanya waombe malipo ya dhamana ya amana bila ya wao kujua.

Continue reading

Mkuu wa FinCEN Ajiuzulu

2 May 2016

Imetangazwa kwamba mkuu wa Idara ya Hazina ya Marekani FinCEN, Jennifer Shasky Calvery anaondoka kwenye idara hiyo. Kutokana na maelezo ya FinCEN, siku yake ya mwisho itakuwa 27 Mai, 2016.

Alijiunga na FinCEN mwaka 2012 na ameiongoza idara hiyo kwenye matatizo ya hivi karibuni ya kuyashambulia mabenki ikiwamo Benki ya FBME, kwa madai kuwa yana mifumo dhaifu ya kupambana na fedha chafu. Madai haya dhidi ya Benki ya FBME yamefunguliwa mashataka kwenye mahakama ya Maerkani.

Inasemekana Bi shasky Calvery anatarajia kujiunga na benki ya HSBC.

Profesa wa Marekani: “Kujiamini kwa Kupitiliza” kwa FinCEN Kunahitaji Usimamizi”

Aprili 16, 2016

 

Akiandika kwenye tovuti ya Amerika Banker, Sharyn O’Halloran, Profesa wa George Blumenthal wa Uchumi Siasa na Profesa wa masuala ya kimataifa na ya umma katika Chuo Kikuu cha Columbia, aliandika kwamba katika vitendo vyake dhidi ya FBME ni wazi kwamba “… Kujiamini kupita kiasi kwa FinCEN kunahitaji uangalizi zaidi” kutoka mamlaka za Marekani. Aliyaelezea mapendekezo ya adhabu ya FinCEN kama ya “kibabe”, na kuonyesha “… mapengo ya dhahiri katika mchakato wake wa utawala na ukosefu wa vielelezo muhimu katika kutekeleza azma yake kwa FBME, (ambayo) inaonyesha kwamba FinCEN ‘walitembea wakiwa wamelala’ kuelekea kwenye maamuzi yaliyopangwa ya kutaka tu taasisi ifungwe “.

Aliongeza kuwa “… inaonyesha pia kwamba kwa FinCEN kuilenga mipaka ya benki ni kinyume cha katiba,” na anaamini kwamba kwa kupinga mashambulizi ya FinCEN, FBME “… ina kesi nzuri”. Makala kamili inapatikana hapa: http://www.americanbanker.com/bankthink/overzealous-fincen-needs-more-oversight-1080438-1.html