Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Cyprus Aishukia Benki Kuu

Aprili 12, 2016

 Mr Alekos Markides, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ambaye sasa ni mshauri wa sheria kwenye Benki ya FBME alifanya mazungumzo kwenye vyombo viwili tofauti vya habari; redio ya taifa CyBC (tar 12 Aprili) na MEGA Television (tar 9 Aprili) katika kukabiliana na uanzishwaji wa hivi karibuni wa Mfuko wa Ulinzi wa Amana. Alidai kuwa Benki Kuu imekosa mkakati na sasa inajaribu kukwepesha mustakabali mzima kutokana na jinsi walivyolishughulikia suala hili.

Continue reading

Uanzishaji wa Mfuko wa Ulinzi wa Amana inailinda CBC, sio Wateja

Aprili 10, 2016

 Kufuatia mfululizo wa vitendo viovu, vilivyo kinyume cha sheria, holela na kukosekana kwa uwajibikaji kwa Benki Kuu ya Cyprus ( “CBC”), na kutangazwa kulikocheleweshwa kwa kuanzishwa mfuko wa ulinzi wa amana Aprili 9, 2016 ni hoja ionayokaribishwa, lakini ni miezi 21 baada ya Mamlaka ya Azimio na CBC kuitekeleza dhidi ya Benki ya FBME ( “FBME”).

Continue reading

Uamuzi wa CBC ni Kinyume cha Sheria na Usiofaa

6 Aprili 2016

Msimamizi Maalum wa Benki ya FBME tawi la Cyprus ametoa barua za kuwaachisha kazi wafanyakazi 136 ili kupunguza gharama na kulinda amana. Sababu alizotoa eti ni kubana matumizi na kulinda amana za wateja?! Hivi sasa Benki ina mtaji na akiba ya dola milioni 162 zaidi ya fedha zinazohitajika kufidia amana zote na gharama yoyote itakatwa kutoka kwenye fedha hizi. Pamoja na hayo, sababu inayosemekana kubana matumizi haina maana yoyote kwa wateja. Hakika, kinyume chake, uwezo wa benki wa kuhifadhi mali zake umeathiriwa vibaya kwa sababu ya kuwapoteza wafanyakazi hawa.

Continue reading

Ufafanuzi: Maamuzi ya Mwisho Yaliyo Mbali na Mwisho

Machi 27, 2016

Maamuzi yanayosemekana kwamba ni ya “Mwisho” yaliyochapishwa na FinCEN Ijumaa, Machi 25, 2016, sio kweli kabisa kwamba ni ya “mwisho”. Bado yapo chini ya amri ya zuio la awali la mahakama ya shirikisho ya Washington DC ambayo inazuia maamuzi haya kufanya kazi na kuleta athari ikisubiri uchunguzi zaidi wa mahakama hiyo katika masuala ya haki, usahihi na uhalali wa mchakato wa FinCEN. “Maamuzi ya Mwisho” pia yana masharti yake yenyewe, kwamba ni lazima yasubiri kipindi cha miezi mine baada ya kuchapishwa rasmi na tarehe ya utekelezaji wa maamuzi hayo. FBME ina haki zote na nia ya kupinga uhalali wa “Maamuzi ya Mwisho” ili mahakama ya Marekani iweze kuamua kama ni halali maamuzi hayo kufanya kazi.

Continue reading

Gavana wa zamani wa CBC Ashangazwa na Maamuzi ya FinCEN

Februari 11, 2016

Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Cyprus (CBC), Profesa Panicos Demetriades, amewaandikia FinCEN kuhusu kampeni yake dhidi ya FBME ambapo anasema “… anashangazwa sana na vitendo vya FinCEN kwa FBME”. Barua hii inaonekana kwenye tovuti ya FinCEN na inapatikana kwa umma kwenye anuani: http://www.regulations.gov/#!documentDetail;D=FINCEN-2014-0007-0069.

Continue reading

Maoni kutoka Kwa Profesa wa Chuo Kikuu cha Columbia

Februari 10, 2016

Maoni zaidi kwenye tovuti ya FinCEN kuhusu jinsi idara hiyo inavyoshughulikia kesi ya FBME, yamewasilishwa na Sharyn O’Halloran, Profesa wa George Blumenthal katika Chuo Kikuu cha Columbia jijini New York. Katika barua yake iliyotumwa kwa FinCEN na kuwekwa kwenye tuvuti ya umma, Profesa O’Halloran alieleza kuwa eneo lake la kitaalamu ni utafiti wa michakato ya utawala ya Marekani, mamlaka ya kisheria na majukumu ya usimamizi.

Continue reading

Rais Ajibu Barua ya Mwenyekiti wa FBME

Januari 19, 2016

Rais wa Jamhuri ya Cyprus, Bw Nicos Anastasiades, ametuma jibu fupi kwa barua ya Desemba 27 kutoka kwa Mwenyekiti wa Benki ya FBME, Ayoub-Farid M Saab (ambayo inaweza kupatikana kwenye tovuti hii).

Akiijibu barua hiyo kutoka Mr Saab, Rais amesema kwamba kwa sababu suala lipo chini ya mahakama si yeye wala waziri yeyote anayeweza “… kuingilia kati, kuzungumzia au kushawishi maamuzi na utaratibu unaoendelea”